Skip to main content

MAFUNZO YA MABADILIKO SHERIA ZA KODI YAANZA MCHINI

Na Cecilia Shiratu, Missenyi - Kagera.

MAFUNZO YA MABADILIKO SHERIA ZA KODI YAANZA MCHINI

Na Cecilia Shiratu, Missenyi - Kagera.

Mafunzo kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2026/2027 yameanza kutekelezwa Julai 1, 2026 Nchini, yakilenga kuwawezesha mawakala wa forodha na watumishi wa mamlaka, kutambua misamaha na taratibu mpya za kodi pamoja na kupanua wigo wa biashara.

Meneja wa Mamlaka ya mapato Nchini (TRA), Mkoa wa Kagera, Joseph Mtalemwa ameyaeleza hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo na kusema utekelezaji wa sheria hiyo unatarajiwa kuongeza idadi ya wafanyabiashara.

Amesema, Wafanyabiashara hao ni wale waliokuwa wakisubiri kupata misamaha ya kodi, huku mafunzo hayo yakifanyika katika maeneo muhimu ya biashara na mipakani, ikiwa ni pamoja na Mutukula, Rusumo, Kabanga na Bandari ya Bukoba.

Naye, Mwezeshaji wa mafunzo hayo Hassan Minga, amesema baadhi ya mabadiliko hayo yanahusu misamaha kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri vinavyotumia nishati pamoja na sekta ya uvuvi, ikiwa ni wazalishaji wa nyavu na wanaoingiza bidhaa hizo nchini.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Marco Gabriel na Godwin Idan wamepongeza na kumshukuru hatua hii ya kutolewa kwa mafunzo hayo nakusema kuwa itawasaidia wafanyabiashara kuelimika na kutambua mabadiliko ya sheria na kutekeleza wajibu wao ipasavyo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.