Na Eunice Kanumba – Shinyanga.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amewataka mafundi ujenzi waweke makubaliano ya kazi hata ikitokea changamoto katika utendaji na kushitakiana, ili iwe rahisi kupata haki, kwa kujenga umoja na mshikamano miongoni mwao,.
Pia mewasisitiza kutumia vifaa vya usalama kazini, kama mavazi ya kiufundi na viatu kwani wengi wao huingia kwenye changamoto zikiwemo za afya na kiusalama kwa kutokutumia vifaa hivyo.

Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, ameyasema hayo kwenye semina ya mafundi ujenzi mkoa wa Shinyanga, iliyoandaliwa na Kampuni ya Magic Builders kwa kuwakutanisha mafundi ujenzi zaidi ya 600.
Amesema, Serikali imechukua jukumu la kuanza kuwatambua mafundi ujenzi na kutaka kuwarasimisha kwa kuwapatia vyeti kupitia chuo cha ufundi stand (VETA) na kwamba kumekuwepo changamoto ya mafundi ujenzi kutopewa kipaumbele na jamii zinazowazunguka na hata inapotokea changamoto ikayopelekea mashitaka katika vyombo vya kisheria wengi hukosa vielelezo vya ushahidi.

"Ufundi salama na ufundi wa ujenzi wenye ujuzi ndiyo unatakiwa na mjithamini kulinda uhai na afya zenu mnapokuwa kazini hakikisheni mnavaa vifaa vya usalama ikiwemo kofia ngumu inaepusha hata ukipata majanga ya kuchomwa na msumari,” amesema Katambi.
Katika hatua nyingine pia amewataka mafundi ujenzi kote nchini kuendelea kuilinda amani ya nchi kwani hata ikitokea vurugu kamwe hawawezi kufanya kazi, hivyo wasikubali kuungana na watu wanaowadanganya na kuwashawishi kufanya vurugu za kuandamana kupitia mitandao ya kijamii.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Magic Builders, David Barongo amesema, mafundi ujenzi walikuwa wamesahaulika ingawa wamekuwa na ujuzi na maarifa na wakitaka kazi mpaka wajieleze na sasa kampuni hiyo imeingia ushirikiano na chuo cha veta kwenda kuwarasmisha mafundi 700,000 nchi nzima.
"Mafundi hawa hawatatoa hata shilingi moja fedha zote zitalipwa na kampuni tumekuwa na programu nyingi lakini haziwalengi mafundi ujenzi tukiwakumbuka wataendelea kutambulisha bidhaa zetu za ujenzi zilizopo sokoni hivi sasa," amesema Barongo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Chuo cha Ufundi (VETA), Rashid Ntahigiye amesema zoezi la kurasimisha makundi mbalimbali lilianza mwaka 2017, hivyo mafundi hao wataanza kurasmishwa na kupatiwa vyeti kwa lengo la utambuzi wa maarifa na ujuzi walioupata nje ya mfumo rasmi.
Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amesema, mafundi ujenzi bado ni Vijana hivyo wanatakiwa wafanye kazi zilizo na faida sio hasara, huku akiwahamasisha kutojiingiza kwenye makundi na kutumika kama hasara ya kuhalibu mali na kukubali kutawaliwa na mamlaka zilizopo, ili waendelee kuwa na maadali.

Baadhi ya mafundi ujenzi akiwemo Emanuel Stephano na Eliud Makala kwa nyakati tofauti wameiambia Jambo Media kuwa elimu iliyotolewa itawasaidia changamoto ya kutoandikishana makubaliano na kudhulumika na kuwasisitiza juu ya uvaaji mavazi maalum ya ufundi na kutotumia vilevi, ili kulinda afya zao.
Discussion
Reader comments
0 contributions