Skip to main content

MAFANIKIO MIRADI YA MAENDELEO HUPIMWA KWA MATOKEO YA MWISHO - DKT. MGANGA

Na Saulo Stephen - Singida.

MAFANIKIO MIRADI YA MAENDELEO HUPIMWA KWA MATOKEO YA MWISHO - DKT. MGANGA
Studio Narration JAMBO FM

MAFANIKIO MIRADI YA MAENDELEO HUPIMWA KWA MATOKEO YA MWISHO...

0:00 --:--

Na Saulo Stephen - Singida.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga, amesisitiza kuwa mafanikio ya miradi ya maendeleo hupimwa kwa matokeo ya mwisho, akieleza kuwa thamani ya fedha inaonekana kupitia ubora wa “finishing” ya miradi.

Amesema ni wajibu wa wasimamizi na wakandarasi kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa viwango vinavyokidhi matarajio na matumizi sahihi ya fedha za umma.

Akitoa maagizo hayo wakati wa ziara ya ukaguzi Wilaya ya Mkalama, Dkt. Mganga alielekeza miradi yote kufuata makadirio ya gharama (BOQ), kuzingatia ubora wa kazi na matumizi sahihi ya rasilimali.

Pia alisisitiza miradi ya afya kuzingatia miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu, kufuata ramani zilizoidhinishwa na kuhakikisha upatikanaji wa maji katika kila chumba cha huduma, akibainisha kuwa huduma ya afya huendana na maji.

Aidha, alisisitiza uwekaji wa vibao vya huduma kwa lugha ya Kiswahili ili kurahisisha mawasiliano kwa wananchi, pamoja na kuimarisha nidhamu ya watumishi kwa kutumia mifumo ya kisasa ya utambuzi (biometric). Vilevile, aliitaka Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kuwasilisha ripoti ya utekelezaji wa miradi yote na kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani.

Katika ziara hiyo, Dkt. Mganga ameendelea na ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya mwaka wa fedha 2025/2026 katika sekta za elimu na afya. Miongoni mwa miradi iliyokaguliwa ni ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Malaja wenye thamani ya shilingi milioni 47.89, ambao umefikia asilimia 72 na unatarajiwa kukamilika Mei 18, 2026.

Miradi mingine ni pamoja na umaliziaji wa maabara mbili katika Shule ya Sekondari St. Benjamini wenye gharama ya shilingi milioni 60.42 unaotarajiwa kukamilika Mei 23, 2026, pamoja na ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Joma lenye thamani ya shilingi milioni 152.8 na uwezo wa kuchukua wanafunzi 80.

Katika sekta ya afya, alikagua ukamilishaji wa Zahanati ya Kotumbili yenye gharama ya jumla ya shilingi milioni 274 itakayohudumia wananchi zaidi ya 3,000, pamoja na Kituo cha Afya Iguguno chenye thamani ya shilingi milioni 250 ambacho kimekamilika katika awamu ya kwanza.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.