Skip to main content

MADURO HATIANI KWA MATESO YA RAIA WA MAREKANI VENEZUELA

Aliyekuwa kiongozi wa Taifa la Venezuela kwa miaka 12 NicolásMaduro Moros amepata shtaka jipya yeye na mke wake, kwa kupanga na kutekeleza mateso dhidi ya raia wa Marekani nchini Venezuela.

MADURO HATIANI KWA MATESO YA RAIA WA MAREKANI VENEZUELA
Studio Narration JAMBO FM

MADURO HATIANI KWA MATESO YA RAIA WA MAREKANI VENEZUELA

0:00 --:--

Aliyekuwa kiongozi wa Taifa la Venezuela kwa miaka 12 NicolásMaduro Moros amepata shtaka jipya yeye na mke wake, kwa kupanga na kutekeleza mateso dhidi ya raia wa Marekani nchini Venezuela.

Kwa mujibu wa arifu za duru nchini Marekani, wawili hao wameshtakiwa na jopo la waendesha mashtaka nchini humo shtaka ambalo linafuata mashtaka ya awali yaliyowakuta na hatia za kuendesha magenge ya biashara za dawa za kulevya na silaha.

Hata hivyo, kufuatia mashtaka hayo Maduro na mkewe Cilia Flores wameyakana yote huku Wakili wa Maduro,Pollack amesema mteja wake ameyakana mashtaka hayo mapya akisubiri nafasi ya kujitetea mahakamani.

Hatua hiyo inakuja kufuatia uvamizi na unyakuzi uliofanyika mapema Januari 3 2026 ukiongozwa na vikosi maalum vya jeshi la Marekani Delta force mjini Caracas Nchini Venezuela, hatua iliyowafanya wawili hao kuwekwa mahabusu Brooklyn, mjini New York.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.