Skip to main content

MADIWANI KYERWA WATAKIWA KUDHIBITI UTOROSHAJI KAHAWA, MIANYA UPOTEVU WA MAPATO

Na Cecilia Shiratu, Kyerwa - Kagera.

MADIWANI KYERWA WATAKIWA KUDHIBITI UTOROSHAJI KAHAWA, MIANYA UPOTEVU WA MAPATO

Na Cecilia Shiratu, Kyerwa - Kagera.

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Zaitun Msofe amewaagiza Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, kuhakikisha wanaongeza nguvu katika kudhibiti utoroshaji wa Kahawa na mianya ya upotevu wa mapato, ambayo yananaathiri uchumi wa Wananchi na Taifa kwa ujumla.

DC Msofe ametoa agizo hilo katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo, kilichojadili namna ya utekelezaji wa shughuli za robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026.

Amesema, Kahawa ni zao muhimu kwa wanachi wa Kyerwa na pia ni chanzo kikubwa cha mapato ya Halmashauri hiyo, hivyo Madiwani wanalo jukumu la kufuatilia biashara ya zao hilo katika maeneo yao na kuhakikisha Wafanyabiashara wanalipa ushuru.

Agizo la DC Msofe linakuja kufuatia baadhi ya Wakulima kuuza Kahawa kwa watu binafsi, ambao huweka mizani majumbani badala ya kuipeleka kwenye Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS), jambo alilosema linaweza kudhoofisha mfumo wa minada.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kyerwa, Bahati Henerico amesema, wamekusanya na kupokea Sh Bilioni 47.1 katika mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo kufikia Juni 2026 Halmashauri imepokea na kukusanya Bilioni 51.1 ambayo ni sawa na asilimia 108 na kuvuka lengo kwa fedha zilizokuwa zimeainishwa.

Amesema, mapato ya ndani yamefikia Sh bilioni 7.9 sawa na asilimia 101 ya lengo la Sh bilioni 7.7.

Hata hivyo, Wakulima na wananchi Wilayani humo wameiomba Serikali kuwapatiwa bei nzuri ya kuuza mazao yao lakini na kulipwa kwa wakati kwenye AMCOS, kwani ucheleweshaji wa malipo huwafanya wawe na changamoto za kifedha na maisha duni kwa uuzaji wa bei ya chini.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.