Skip to main content

MADIWANI FANYENI MIKUTANO KUSIKILIZA, KUTATUA KERO ZA WANANCHI - DC NKINDA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

MADIWANI FANYENI MIKUTANO KUSIKILIZA, KUTATUA KERO ZA WANANCHI - DC NKINDA
Studio Narration JAMBO FM

MADIWANI FANYENI MIKUTANO KUSIKILIZA, KUTATUA KERO ZA WANANC...

0:00 --:--

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

Madiwani katika manispaa ya kahama mkoani Shinyanga  wametakiwa kufanya mikutano katika kata zao, ili kusikiliza na kutatua kero za wananchi ambao wengi wao wanakosa sehemu ya kufikisha kero hizo.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda kwenye kikao cha kawaida cha robo ya tatu cha baraza la madiwani la manispaa hiyo kilichofanyika kwenye ukumbi wa manispaa hiyo.

Nkinda amesema kuwa mikutano hiyo ni muhimu kwani inawapa fursa wananchi kueleza kero zao na kufahamu utekelezaji w ilani ya uchaguzi katika maeneo yao na kwamba kila anpofanya mikutano anapokea kero nyingi za wananchi hao.

“Waheshimiwa madiwani niwaombe mfanya mikutano ya kusikiliza kero za wananchi katika kata zenu,Mikutano hii inawapa dira wananchi kujua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na inapunguza  maswali kwa viongozi wanapotembelea katika kata zenu” Amesema Nkinda.

Nkinda amesema kuwa katika maeneo mengi anayopita kufanya mikutano anakutana na kero nyingi za wananchi hali inayoonesha madiwani hawafanyi mikutano katika maeneo yao hali inayosababisha ukosefu wa ushirikishwaji baina ya wananchi na viongozi.

“Mimi nafanya mikutano katika maeneo tofautitofauti ,nakutana na kero nyingi toka kwa wananchi ambayo ukiiangalia kero zingine zinaweza kumalizwa na diwani,sasa hii inaonesha kwamba baadhi ya madiwani hamfanyi mikutano kabisa katika maeneo yenu” Amesisitiza Nkinda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Kahama Thomas Muyonga amesisitiza ushirikiano kati ya viongozi na wananchi na kwamba utasaidia kuharakisha utatuzi wa changamoto mbalimbali na kuimarisha maendeleo ya jamii.

“Tunapoenda kusikiliza kero za wananchi tunakuza ushirikiano kati ya viongozi na jamii amba oni wananchi,lakini hii itasaidia kuharakisha utatuzi wa changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi katika maeneo yao,kwahiyo nendeni mkafanye mikutano kama tulivyowakabidhi ilani ya chama cha mapinduzi” Amesema Muyonga.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.