Skip to main content

MADINI YA BILIONI 3.3 YAKAMATWA KATIKA MATUKIO 55 YA USAFIRISHAJI HARAMU

Na Clavery Christian, Bukoba - Kagera.

MADINI YA BILIONI 3.3 YAKAMATWA KATIKA MATUKIO 55 YA USAFIRISHAJI HARAMU

Na Clavery Christian, Bukoba - Kagera.

Madini yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 3.3 yamekamatwa katika matukio 55 ya usafirishaji haramu yaliyobainika nchini kati ya Julai 2025 na Machi 2026, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kudhibiti biashara haramu ya madini na kulinda rasilimali za taifa.

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, alisema kuwa kati ya Juni na Julai 2026, mkoa wa Kagera pekee ulikuwa na ukamataji wa madini na vito vya dhahabu vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.4.

Alieleza kuwa operesheni hizo zilifanikisha kukamatwa kwa dhahabu iliyokuwa ikisafirishwa kinyume cha sheria kupitia eneo la Benako, wilayani Ngara. Miongoni mwa mizigo iliyokamatwa ni dhahabu yenye uzito wa gramu 4,434.66, yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.3, ambayo ilikuwa ikielekezwa mpaka wa Rusumo bila kibali cha kisheria.

Dkt. Kiruswa alisema Serikali itaendelea kuimarisha usimamizi wa sekta ya madini na kuchukua hatua kali dhidi ya wote wanaojihusisha na biashara haramu ya madini.

Aidha, alibainisha kuwa watuhumiwa wote waliohusika na matukio hayo wamefikishwa mahakamani, huku kesi zao zikiendelea kusikilizwa kwa mujibu wa sheria.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.