Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Kanda ya Kati imetoa elimu Kwa Wanafunzi wa shule mbalimbali mkoani Singida.
Elimu hiyo imetolewa katika shule ya Msingi Sabasaba, Utemini, Bomani, Unyankindi, Mesomapya, Muhalala, Mlewa, Kimadoi, Mji Mpya na Mwanzi Sekondari .

Katika kampeni hiyo, zaidi ya wanafunzi 10,500, walipatiwa elimu juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya na mbinu za kutokuingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
DCEA imekuwa ikisisitiza kuwa Matumizi ya dawa tiba zenye asili ya Kulevya kama mbadala wa dawa za kulevya, bila ushauri wa mtaalamu wa afya, kwa kipimo kisichopendekezwa au kwa lengo la kupata athari za kulevya, zinaweza kusababisha utegemezi, kuathiri mfumo wa fahamu na kusababisha madhara makubwa kiafya.
Discussion
Reader comments
0 contributions