Skip to main content

MABADILIKO YA SERA ZA KIMATAIFA:NGO'S GEITA ZAKOSA BILIONI 6 ZA UFADHILI WA MIRADI

Kufuatia dunia kushuhudia mabadiliko ya sera za Kimataifa,katika Taifa la Marekani yaliyoathiri ufadhili wa miradi ya Maendeleo katika nchi zinazoendelea,mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoani Geita yamepoteza ufadhili wa kiasi cha shilingi bilioni 6 zilizotarajiwa kutumika kutekeleza miradi mbalimbali.

MABADILIKO YA SERA ZA KIMATAIFA:NGO'S GEITA ZAKOSA BILIONI 6 ZA UFADHILI WA MIRADI
Studio Narration JAMBO FM

MABADILIKO YA SERA ZA KIMATAIFA:NGO'S GEITA ZAKOSA BILIONI 6...

0:00 --:--

Kufuatia dunia kushuhudia mabadiliko ya sera za Kimataifa,katika Taifa la Marekani yaliyoathiri ufadhili wa miradi ya Maendeleo katika nchi zinazoendelea,mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoani Geita yamepoteza ufadhili wa kiasi cha shilingi bilioni 6 zilizotarajiwa kutumika kutekeleza miradi mbalimbali.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la mashirika yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) Mkoa wa Geita,Bi Paulina Alex Majogolo amebainisha hayo katika mkutano wa Jukwaa la mwaka la mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Geita akibainisha kuwa kutokana na upungufu huo wa fedha kazi mbalimbali za mashirika hayo ndani ya jamii zimeathiriwa.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) Mkoa wa Geita,Bi Paulina Alex Majogolo.(Picha na Ibrahim Rojala)

“Hii imesababisha changamoto kubwa kwa walengwa wakubwa ambao tulikuwa tunawahudumia aidha kupunguza misaada kwao au kusitisha kabisa huduma kwao”amesema Bi.Paulina

Akizungumza katika Jukwaa hilo,Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita,Herman Matemu ameeleza kwamba Mkoa huo una jumla ya mashirika 112 yasiyo ya Kiserikali yaliyosajiliwa na yenye makao makuu Mkoani Geita lakini ni machache kati ya hayo yaliyo na miradi ndani ya jamii baada ya kusajiliwa.

“Hii inatokana na utegemezi wa fedha za wahisani hali inayosababisha kuzorota kwa utoaji wa huduma na uchangiaji wa wa maendeleo endelevu na ustawi wa jamii kwa ujumla”amesema Matemu

Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita,Herman Matemu akitoa hutuba katika Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's)Mkoa wa Geita.(Picha na Ibrahim Rojala)

Matemu ameeleza kwamba Serikali itaendelea kushirikiana na mashirika yasiyo ya Kiserikali katika utoaji wa huduma mbalimbali ndani ya Mkoa wa Geita kutokana na ukweli kwamba serikali haiwezi kupita kila mahali na kufikisha huduma za kijamii kwa wakati mmoja.

“Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita inatambua mchango na kazi kubwa inayofanywa na mashirika yasiyo ya Kiserikali ili kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta mbalimbali ambazo ni elimu,afya,kilimo ,mifugo,msaada wa kisheria, mazingira, utokomezaji wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto,mapambano dhidi ya VVU\UKIMWI,kupinga mila na desturi zenye madhara katika jamii,kusaidia watu wenye ulemavu pamoja na kuwezesha wananchi kiuchumi ndani ya Mkoa wa Geita”ameeleza Matemu

Akitolea mfano wa hali ya mambo ilivyo Wilayani Nyang’hwale,Msajili Msaidizi wa mashirika yasiyo ya Kiserikali wa Wilaya hiyo,Samweli Charles Murango amesema hali hiyo imepelekea baadhi ya mashirika ndani ya Wilaya hiyo kushindwa kulipa watumishi na mengine kushindwa kutekeleza miradi ambayo ilikuwa na manufaa kwa jamii.

Kutokana na uwepo wa changamoto hiyo Afisa Miradi Msaidizi wa Shirika la NELICO Agatha Boniface Lushinge amesema mashirika yanapaswa kuanzisha miradi ya uzalishaji itakayoyawezesha kumudu gharama za uendeshaji wa miradi ya kijamii pamoja na kufanya kazi kwa ubia.

Kwa upande wake Mratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Geita Martha Philipo Kaloso ameyataka mashirika hayo kuzingatia taratibu ikiwa ni pamoja na kujitambulisha kwa viongozi wa Serikali za mitaa na vijiji katika maeneo wanayotekeleza miradi,utoaji wa taarifa za utekelezaji wa miradi kwa Serikali na kushirikiana na viongozi wote katika hatua za utekelezaji wa miradi hiyo.

Mratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Geita,Martha Philipo Kaloso akiwasilisha mada katika Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Geita.(Picha na Ibrahim Rojala)

Jukwaa la Mwaka la Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali Mkoa wa Geita limefanyika chini ya kaulimbiu isemayo;Fikra mpya Kuhusu Uendelevu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali,Ubunifu Ubia na Upatikanaji wa Rasilimali Fedha kupitia vyanzo vya ndani.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.