Skip to main content

MABADILIKO YA DUNIA NI FURSA ZA KIMAENDELEO - DKT. MWIGULU

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Afrika inapaswa kutumia mabadiliko yanayoendelea katika siasa, uchumi na usalama duniani kama fursa ya kuharakisha maendeleo yake.

MABADILIKO YA DUNIA NI FURSA ZA KIMAENDELEO - DKT. MWIGULU

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Afrika inapaswa kutumia mabadiliko yanayoendelea katika siasa, uchumi na usalama duniani kama fursa ya kuharakisha maendeleo yake.

Amesema inapaswa kufanya hivyo kwa kuimarisha uongozi wa kimkakati, kuongeza thamani ya rasilimali zake na kujenga taasisi imara zitakazolinda maslahi ya wananchi wake na kuharakisha maendeleo ya Bara la Afrika.

“Afrika isiendelee kuwa uwanja wa ushindani wa mataifa makubwa. Tunapaswa kutumia nafasi yetu ya kimkakati, rasilimali tulizonazo na nguvu ya watu wetu kujiletea maendeleo yenye manufaa kwa wananchi wetu,” amesema.

Waziri Mkuu alisema hayo leo Julai 21, 2026 katika Mkutano wa Pili wa Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (National Defence College – Tanzania) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Alisema dunia inaendelea kushuhudia mabadiliko makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama yanayochochewa na ushindani wa mataifa makubwa, maendeleo ya teknolojia, mabadiliko ya nishati na ushindani wa rasilimali muhimu, hali inayozitaka nchi za Afrika kuwa na viongozi wenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kimkakati kwa manufaa ya Bara.

Alisisitiza Afrika ina takribani asilimia 30 ya madini muhimu yanayohitajika katika mapinduzi ya teknolojia na nishati safi duniani, hivyo Bara hilo linapaswa kutumia nafasi hiyo kujenga uchumi imara kupitia kuongeza thamani ya rasilimali zake badala ya kuendelea kuuza malighafi na kutegemea mataifa mengine.

“Afrika lazima iache kuwa uwanja wa ushindani wa mataifa makubwa. Tunapaswa kujenga uwezo wa kuongeza thamani ya rasilimali zetu, kuimarisha biashara ndani ya Bara na kutumia fursa zilizopo kujenga uchumi shindani na endelevu,” alisisitiza.

Aidha, Waziri Mkuu amesema viongozi wa Afrika wanapaswa kujenga taasisi zenye uwezo wa kusimamia maendeleo, kulinda maslahi ya wananchi na kuhakikisha rasilimali za Bara zinatumika kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.