Na Clavery Christian, Bukoba - Kagera.
Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) Mkoa wa Kagera wamepewa mafunzo kuhusu matumizi ya mfumo wa TANCIS unaotumika katika vituo vya forodha vya mkoa huo kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika sekta ya forodha.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyowakutanisha mawakala na maafisa waliopo makao makuu ya TRA Mkoa wa Kagera, Meneja Msaidizi wa Forodha Mkoa wa Kagera, Hery Talawa amesema mafunzo hayo yatafanyika kwa muda wa siku tano.

Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwafikia watumiaji wa huduma za forodha pamoja na wananchi kwa ujumla ili kuongeza uelewa wa matumizi ya mfumo huo na kuendelea kuondoa changamoto zinazojitokeza katika utoaji wa huduma.
Kwa upande wake, Afisa Forodha Mkuu January Shauri amesema mfumo wa TANCIS unatumiwa na nchi wanachama wa Afrika Mashariki katika utoaji wa vibali vya forodha, ikiwemo Tanzania, kwa kufuata sheria ya mwaka 2004 iliyofanyiwa maboresho mwaka 2011 pamoja na kanuni zake.

Ameeleza kuwa matumizi ya mfumo huo yamelenga kupunguza ucheleweshaji wa huduma katika idara mbalimbali na kuongeza ufanisi katika shughuli za forodha na biashara mipakani.
Mafunzo hayo pia yanatarajiwa kufanyika katika Elaya za Karagwe District, Kyerwa District, Missenyi District na Ngara District ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo maafisa pamoja na wadau wa forodha.

Discussion
Reader comments
0 contributions