Skip to main content

MAAFISA MAENDELEO SHYDC WASAFISHA MAZINGIRA, KUTOA MSAADA KITUO CHA AFYA NINDO

Umoja wa Maafisa Maendeleo wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wamefanya zoezi la usafi pamoja na kugawa mahitaji mbalimbali kwa wazazi katika Kituo cha Afya Nindo, ikiwa ni sehemu ya kilele cha Mwezi wa Maafisa Maendeleo ndani ya halmashauri hiyo.

MAAFISA MAENDELEO SHYDC WASAFISHA MAZINGIRA, KUTOA  MSAADA KITUO CHA AFYA NINDO
Studio Narration JAMBO FM

MAAFISA MAENDELEO SHYDC WASAFISHA MAZINGIRA, KUTOA MSAADA K...

0:00 --:--

Umoja wa Maafisa Maendeleo wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wamefanya zoezi la usafi pamoja na kugawa mahitaji mbalimbali kwa wazazi katika Kituo cha Afya Nindo, ikiwa ni sehemu ya kilele cha Mwezi wa Maafisa Maendeleo ndani ya halmashauri hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Kitengo cha Divisheni ya Utumishi wa Umma, Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Kata ya Mwalukwa Elpendo John, amesema hatua hiyo inalenga kuwa mfano hai wa kuigwa na jamii, huku akiwataka wananchi kuendelea kufanya usafi katika maeneo yao, ili kujikinga na madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha kuanzia mwezi Oktoba.

KAIMU MKUU WA KITENGO CHA DIVISHENI YA UTUMISHI WA UMMA ELPENDO JOHN

Sambamba na hilo, Afisa Afya wa Kituo cha Afya Nindo, Jibril Adam, kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, amepongeza Umoja huo chini ya Mkuu wa Kitengo cha Divisheni ya Utumishi wa Umma wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa msaada walioutoa, pamoja na kuhamasisha utunzaji wa mazingira kupitia zoezi la usafi.

Amesema Umoja huo ni mfano wa kuigwa na taasisi mbalimbali ndani na Mkoa wa Shinyanga na taifa zima kwa ujumla.

Aidha, Afisa huyo amesema msaada uliotolewa kwa wazazi katika kituo hicho utawasaidia kutekeleza majukumu ya malezi na matunzo ya watoto, kwa kuwa baadhi ya wazazi hushindwa kumudu gharama za mahitaji kutokana na hali duni ya maisha.

Nao baadhi ya wazazi katika kituo hicho, akiwemo Getruda Juma na Elizabeth Mathias, wameeleza kufurahishwa na hatua iliyofikiwa na Umoja huo, wakisema msaada huo utawasaidia wazazi ambao wakati mwingine hushindwa kumudu gharama za mahitaji mbalimbali pindi wanapojifungua.

UMOJA WA MAAFISA USTAWI WAKIKABIDHI ZAWADI KWA WAGONJWA KATIKA KITUO CHA AFYA NINDO

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.