Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema kuwa kesi ya uhaini inayomkabili katika Mahakama Kuu, inatarajiwa kufikia hatua muhimu hivi karibuni.
Lissu amesema hayo hii leo Agosti 26, 2026 akiwa Mahakamani wakati akizungumza na Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika pamoja na Makamu wake, John Heche.
Aidha, Lissu pia anatarajiwa kuhitimisha sehemu ya kwanza ya ushahidi wa utetezi wake katika kesi ya uhaini inayomkabili, ikiwa ni siku ya tatu mfululizo kwa kutoa ushahidi wake katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es salaam.

Mara baada ya kukamilisha ushahidi wake, hatua itakayofuata itakuwa ni "cross-examination" ambapo Lissu atahojwa na Waendesha Mashtaka kuhusu ushahidi alioutoa.
Kesi hiyo inasikilizwa na Jopo la Majaji watatu, wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akisaidiana na Majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.
Discussion
Reader comments
0 contributions