Skip to main content

LISSU AANGUKIA PUA TUZO YA HAKI ZA BINADAMU 2026

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na maafisa wake wameshinda Tuzo ya Haki za Binadamu ya Sakharov ya mwaka 2026, wakimbwaga Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, aliyekuwa miongoni mwa wanaowania tuzo hiyo.

LISSU AANGUKIA PUA TUZO YA HAKI ZA BINADAMU 2026
Studio Narration JAMBO FM

LISSU AANGUKIA PUA TUZO YA HAKI ZA BINADAMU 2026

0:00 --:--

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na maafisa wake wameshinda Tuzo ya Haki za Binadamu ya Sakharov ya mwaka 2026, wakimbwaga Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, aliyekuwa miongoni mwa wanaowania tuzo hiyo.

Lissu, alikuwa miongoni mwa watatu wanaowania tuzo hiyo, ameangukia pua. Wengine walioshindwa pamoja na Lissu ni raia wa Iran Taraneh na Romina Rahimi.

Akimtangaza mshindi, Rais wa Bunge la Ulaya, Roberta Metsola, amesema ICC imeshinda kutokana na umahiri wake katika kulinda sheria za kimataifa na haki.

Amesema ICC huchunguza na kufikisha mahakamani watu wanaotuhumiwa kutenda makosa makubwa, yakiwamo mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Tuzo hiyo iliyoanzishwa mwaka 1988 kwa heshima ya Andrei Sakharov, hutolewa kila mwaka kwa watu au taasisi zinazotetea haki za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.