Skip to main content

LESENI TISA ZA UTAFITI WA MADINI ZATOLEWA KWA KAMPUNI YA SAUDI ARABIA

Serikali imetoa leseni tisa za utafiti wa madini kwa kampuni ya Saudi Gold Refinery kutoka Saudi Arabia, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuvutia uwekezaji na kuongeza shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini nchini.

LESENI TISA ZA UTAFITI WA MADINI ZATOLEWA KWA KAMPUNI YA SAUDI ARABIA

Serikali imetoa leseni tisa za utafiti wa madini kwa kampuni ya Saudi Gold Refinery kutoka Saudi Arabia, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuvutia uwekezaji na kuongeza shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema utoaji wa leseni hizo umetokana na dhamira ya kampuni hiyo kuwekeza nchini, kufuatia mkutano wa kibiashara kati ya Tanzania na Saudi Arabia uliofanyika Dar es Salaam.

Mavunde amesema katika mkutano huo, kampuni hiyo ilionesha nia ya kuwekeza katika sekta ya madini, huku Serikali ikiahidi kuwezesha upatikanaji wa leseni za awali ndani ya siku saba za kazi, ahadi ambayo imetekelezwa.

Amesema kampuni hiyo imeendelea kuomba maeneo mengine kwa ajili ya utafiti kupitia Tume ya Madini kutokana na fursa za uwekezaji zilizopo nchini.

Ameeleza kuwa Serikali imeipa kampuni hiyo fursa kutokana na uwezo wake wa kifedha, teknolojia na utaalamu wa kufanya utafiti wa kina wa madini.

Aidha, amesema Serikali inaendelea kupitia leseni za madini ambazo zimekuwa zikishikiliwa bila kufanyiwa kazi, na kwamba maeneo yatakayobainika kutotumika yatarejeshwa Serikalini na kutolewa kwa wawekezaji wenye uwezo na dhamira ya kuyaendeleza.

Mavunde ameongeza kuwa baadhi ya maeneo hayo yatafungua fursa kwa wawekezaji wengine na wachimbaji wadogo, wakiwemo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kupitia programu ya Mining for Brighter Tomorrow. Wizara ya Madini- Ministry of Minerals,Tanzania Anthony Mavunde

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.