Skip to main content

LAMI 'YANUKIA' KWIMBA-MWANZA, BILIONI 5.5 ZATENGWA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, CP Salum Hamduni, amesema Serikali ina mpango wa kuiunganisha Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba na Makao Makuu ya Mkoa kwa barabara za lami, huku akiahidi kuongeza nguvu, ili kuhakikisha fedha za miradi hiyo zinapatikana kwa wakati.

LAMI 'YANUKIA' KWIMBA-MWANZA, BILIONI 5.5 ZATENGWA
Studio Narration JAMBO FM

LAMI 'YANUKIA' KWIMBA-MWANZA, BILIONI 5.5 ZATENGWA

0:00 --:--

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, CP Salum Hamduni, amesema Serikali ina mpango wa kuiunganisha Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba na Makao Makuu ya Mkoa kwa barabara za lami, huku akiahidi kuongeza nguvu, ili kuhakikisha fedha za miradi hiyo zinapatikana kwa wakati.

Mhe. Hamduni ameyasema hayo leo tarehe 28 Septemba, 2026, wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba katika kikao cha kujitambulisha, kufuatia uteuzi wake alioupata mwishoni mwa mwezi Agosti, 2026. Amesema tayari Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 5.5 kwa ajili ya ujenzi wa barabara tatu muhimu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mhe. Ngh'wilabuzu Ludigija, akitoa salamu za wananchi, ameishukuru Serikali ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga zaidi ya Shilingi Bilioni 6 kwa ajili ya kubadilisha bomba chakavu linalosafirisha maji kutoka Ziwa Victoria.

Aidha, Mhe. Ludigija ameishukuru Serikali kwa kuimarisha sekta ya Elimu wilayani humo kwa kuajiri walimu wapya zaidi ya 250 wa Elimu ya Msingi na Sekondari ndani ya siku 100 tu baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.