Kumbukumbu zinatuonesha kuwa leo Novemba 3, kuna historia nyingi duniani mbali na Siku ya Wanahabari, ambazo ziliwahi kutukia na kuacha alama.
Hapa nakusogezea historia kubwa za Novemba 3, ambazo bado zinaishi na kufanya wale wapenda kujifunza wapate manufaa kielimu.

1957 - Mbwa wa Kwanza Angani:
Urusi ilirusha Sputnik 2 ikiwa na mbwa Laika, mnyama wa kwanza kuzunguka dunia. Alitoka mitaani Moscow na historia yake ilifungua njia ya safari za binadamu angani.
Ipo hivi, Mbwa huyu ndiye kiumbe wa kwanza kutoka nje ya Dunia kama sehemu ya Jaribio mnamo 3 November 1957, kisha akafia huko baada baada ya chombo kufika huko Anga za mbali kwa kukosa hewa safi ya Oksijeni.

Hiyo ikawa sababu ya Wanasayansi kugundua kwamba huko hakuna hewa ya Oksijeni, ndipo wakagundua mbinu ya kwenda Anga za mbali kwamba ni lazima ubebe Oxygen kama vile unazama Baharini.
1903 - Panama inapata Uhuru:
Panama ilitangaza kujitenga kutoka Colombia baada ya mapinduzi yaliyoungwa mkono na Marekani ili kupisha ujenzi wa Mfereji wa Panama
1911 - Chevrolet inazaliwa:
Kampuni ya magari ya Chevrolet ilianzishwa na dereva Louis Chevrolet na William Durant
1978 - Dominica Uhuru:
Kisiwa cha Dominica Caribbean kilipata uhuru kutoka Uingereza.

1534 - Mfalme Henry VIII:
Bunge la Uingereza lilipitisha sheria ya kumfanya Mfalme Henry VIII kuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Uingereza, akijitenga na Roma
2014 - One World Trade Center inafunguliwa:
Jengo refu la One World Trade Center lilifunguliwa New York, miaka 13 baada ya mashambulizi ya Sept 11 ef4a82a3cccf4e4c
Na leo pia ni National Sandwich Day na World Jellyfish Day duniani.
Discussion
Reader comments
0 contributions