Skip to main content

KUWASA YAWEKA MKAKATI WA MIAKA MITANO KUBORESHA HUDUMA KAHAMA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

KUWASA YAWEKA MKAKATI WA MIAKA MITANO KUBORESHA HUDUMA KAHAMA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Kahama (KUWASA) imeweka mkakati wa miaka mitano ya huduma ya utoaji wa maji kwa wananchi kuanzia 2026 hadi 2031 ikiwa na lengo la kuboresha upatikanaji wa  huduma hiyo kwa wananchi.

Akizungumza kuhusu mpango wa mamlaka hiyo kwa kipindi cha miaka 5, Kaimu mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na uhusiano kwa Umma (KUWASA) John Mkama amesema kuwa mpango huo umelenga kupanua miundombinu ya maji kwa kilometa 83 ili kuwafikia watu wanaohitaji huduma ya maji kwa kata zote Pamoja na Kununua dira mpya za maji 25000 kati ya hizo dira 1000 ni dira za lipa kabla (Smart Meter).

“Tunayo malengo mengi ya mpango huu lakini kubwa zaidi ni kupanua miundombinu ya maji kwa kiliometa 83,ikiwa ni Pamoja na kununua dira mpya 25,000 kati ya hizo dira 1000 ni za lipa kabla Pamoja na kukarabati mradi wa maji taka ulipo eneo la Busoka kwa asilimia 100,” amesema Mkama.

Mkama ameongeza kuwa Mpango huo pia umelenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa zaidi ya 85%  masaa 24 kwa siku ikiwa ni Pamoja na kuimarisha mapato na usimamizi wa fedha kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kielektroniki.

“Mpango huu pia umelenga kuboresha upatikani wa maji kwa asilimia 85 yani saa 24 kwa siku lakini pia ni Pamoja na kuimarisha mapato na usimamizi wa fedha kwa njia ya kielekroniki,” ameongeza Mkama.

Awali akizungumza katika kikao hicho Kaimu mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Adam Mgongwa amesema kuwa lengo la kuwaalika wadau ni kuwashirikisha ili watoe maoni yao kwani mamlaka ya maji KUWASA ni taasisi shirikishi inayofanya kazi wa uwazi.

“KUWASA ni taasisi ya Umma hivyo Lengo la kuwaarika wadau wa huduma ya maji katika mkutano huu ni kwamba tunataka kupokea maoni yao ili kuzidi kuboresha huduma ya utoaji wa maji katika mpango wa miaka mitano ijayo” Amesema Mgongwa.

Nao baadhi ya wadau walioshiriki kikao hicho wameiomba mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Kahama (KUWASA) wapunguze gharama za huduma ya gari ya maji taka Pamoja na kuzingatia ukarabati wa haraka wa mabomba yanayopasuka ambayo yanatolewa taarifa na wananchi.

“Kuwasa mnatoa huduma kwa umma lakini bei ya gari lenu la maji taka ni kubwa kama wafanyabiashara wengine,wananchi hawawezi kuacha kutiririsha maji ikiwa gharama ni kubwa,lakini hili la upotevu wa maji tunaomba zingatieni ukarabati wa mabomba yanayopasuka ambayo yanatolewa taarifa na wananchi,” amesema Laurent Nkwabi

Kikao cha wadau wa maji kiliachoandaliwa na mamlaka ya  maji safi na usafi wa mazingira Kahama (KUWASA) imekutanisha wadau kutoka sekta mbalimbali zikiwemo taasisi,watu binafsi,ofisi za umma,wananchi wa kawaida Pamoja na watumishi wa mamlaka hiyo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.