Skip to main content

KUWASA: MAAFISA MAENDELEO KOMESHENI UTIRIRISHAJI MAJI TAKA KAHAMA

Na William Bundala-Kahama Shinyanga

KUWASA: MAAFISA MAENDELEO KOMESHENI UTIRIRISHAJI MAJI TAKA KAHAMA

Na William Bundala-Kahama Shinyanga

Maafisa maendeleo wa kata katika manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kusimamia usafi wa mazingira kwa kukomesha tabia ya baadhi ya wananchi wa manispaa hiyo kutiririsha maji taka ya chooni pindi mashimo yanapojaa.

Wito huo umetolewa leo na afisa uhusiano wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Kahama (KUWASA) John Mkama katika kikao cha wadau cha kujadili mipango ya utekelezaji wa shughuli za mamlaka hiyo.

Mkama amesema kuwa mamlaka inatoa huduma ya maji safi na salama lakini pia inashughurika na usafi wa mazingira na wametenga eneo maalumu la kumwaga maji taka katika eneo la Busoka.

“Mamlaka imetenga eneo maalum kwa ajili ya kukusanya maji taka,ila wapo baadhi ya wananchi wanatitirisha maji taka katika mitaa,Tuwaombe maafisa maendeleo ya kata simamieni na mkemee vitendo hivi vya utiririshaji wa maji taka,kuna magari ya kusomba maji taka na Kwenda kuyatunza sehemu husika hali hii itasaidia kuweka manispaa yetu katika hali ya usafi,” smesema Mkama.

Katika hatua nyingine mkama ameelezea hali ya upotevu wa maji unaotokana na baadhi ya wananchi kuiba maji nyakati za usiku,Kupasuka kwa mabomba na wengine kujiunganishia maji na kufanya kilimo cha umwagiliaji na kutoa wito kwa wananchi kuwa walinzi wa miundo mbinu ya maji.

“Manispaa ya Kahama tunakutana na changamoto kubwa ya upotevu wa maji hii ni kutokana na baadhi ya wananchi kuiba maji nyakati za usiku,mabomba kupasuka kila kukicha pamoja na wengine kujiunganishia maji kwa kufanya kilimo cha umwagiliaji, Hivyo tuombe wananchi tuwe walinzi wa miundombinu yetu na toeni taarifa za siri ili kuwabaini waharibifu,” ameongezea Mkama.

Awali akizungumza katika kikao hicho Kaimu mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Adam Mgongwa amesema kuwa lengo la kuwaalika wadau ni kuwashirikisha ili watoe maoni yao kwani mamlaka ya maji KUWASA ni taasisi shirikishi inayofanya kazi wa uwazi.

“KUWASA ni taasisi ya Umma hivyo Lengo la kuwaarika wadau wa huduma ya maji katika mkutano huu ni kwamba tunataka kupokea maoni yao ili kuzidi kuboresha huduma ya utoaji wa maji katika mpango wa miaka mitano ijayo,” Amesema Mgongwa.

Nao baadhi ya wadau walioshiriki kikao hicho wameiomba mamlaka yam aji safi na usafi wa mazingira Kahama (KUWASA) wapungeze gharama za huduma ya gari ya maji taka Pamoja na kuzingatia ukarabati wa haraka wa mabomba yanayopasuka ambayo yanatolewa taarifa na wananchi.

“Kuwasa mnatoa huduma kwa umma lakini bei ya gari lenu la maji taka ni kubwa kama wafanyabiashara wengine,wananchi hawawezi kuacha kutiririsha maji ikiwa gharama ni kubwa,lakini hili la upotevu wa maji tunaomba zingatieni ukarabati wa mabomba yanayopasuka ambayo yanatolewa taarifa na wananchi,” amesema Laurent Nkwabi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.