Machi 9, 2024 nilimsikia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akiongea na waandishi wa Habari ofisini kwake juu ya maadhimisho ya jubilee ya miaka 25 toka kuondoka kwa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Sendiga alisema kuwa maadhimisho hayo yaliyopewa jina "Tanzania Big Talk" kitaifa yamebeba kauli mbiu ya kuwakumbusha watanzania kutafakari mashujaa wa nchi hii na Bara la Afrika kwa ujumla.
Alisema jukwaa hilo lisilo la kiserikali liamua kushirikiana na Mkoa wa Manyara kuandaa kongamano kubwa la kitaifa, ili kumtafakari hayati Baba wa Taifa hili katika kuenzi utumishi wake kwa Taifa na Bara la Afrika.
Mjadala huo ulibeba mada isemayo "Nyerere the unsung hero of Afrika", yaani (Nyerere shujaa wa Afrika asiyeimbika) ukilenga kuwawezesha vijana, ili wapate nafasi ya kutoa fikra zao juu ya wanavyowafikiria na kuenzi ukuu wa viongozi hao.

Queen Sendiga kwa kutumia kauli ya "Shughuli ni watu na watu wenyewe ndiyo sisi" akasisitiza kuwa 'Uwajibikaji ni rafiki wa Maendeleo', akikazia mchango wa Mwl. Nyerere katika kutumikoq taifa kuleta maendeleo.
WASIFU WA BABA WA TAIFA, JULIUS KAMBARAGE NYERERE:
Tarehe ya kuzaliwa: 13 Aprili 1922
Mahali pa kuzaliwa: Butiama
Tarehe ya kifo: 14 Oktoba 1999
Rais wa kwanza wa Tanzania: Alingia ofisini 1964 - 1985
Alifuatwa na: Ali Hassan Mwinyi
Dini: Mkristo Mkatoliki
Elimu yake Chuo Kikuu cha Edinburgh - Uskoti Digrii anazoshika M.A. ya historia na uchumi. Kazi mwalimu, mwanasiasa.
Nyerere alikuwa mwenyekiti wa chama cha TANU na baadaye wa CCM. Mara nyingi aliitwa "Mwalimu Nyerere". Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania.
Alizaliwa Butiama, mkoani Mara pembezoni mwa Ziwa Nyanza tarehe 13 Aprili, 1922.
Alifariki dunia 14 Oktoba, 1999. Aliiongoza Tanzania toka mwaka 1961 hadi mwaka 1985.
Yeye ni mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea. Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimu.
Kazi hii ndiyo ilimpatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la "Mwalimu." Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiyari baada ya kutawala kwa muda mrefu. Alipostaafu urais mwaka
1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo. Aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.

Maisha Ya Mwalimu
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 (katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika).
Alikuwa mojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya babake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma.
Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusoma shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora.
Ni mengi amelitendwa Taifa hili na hata nukiu zake nyingi bado zinaishi, lakini kubwa zaidi aliwahi kusema "Taifa lisilo na utamaduni wake ni Taifa mfu."
WATANZANIA TUUENZI UTAMADUNI WETU.
Discussion
Reader comments
0 contributions