Na Ibrahim Rojala, Chato - Geita.
Askofu wa Jimbo Katoliki Bunda, Mhashamu Simon Chibuga Masondole amesisitiza umuhimu wa kujenga utamaduni wa kupenda kazi, hatua ambayo ameieleza kuwa ni sadaka kwa Mungu.
Mqsongole ameyasema hayo wakati akizungumza kupitia hotuba ya Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Miaka mitanoya Kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Amesema, "tunafanya kumbukumbu hii kwasababu mambo mengi aliyoyafanya Rais Magufuli hayajaandikwa,na kama yameandikwa hatuyasomi,kwa nyakati hizi huenda pia tumepoteza utaratibu wa kupenda kusoma."
Aidha, ametoa rai kwa viongozi kutumika vyema katika ulinzi wa mipaka ya nchi,akieleza kuwa wananchi wanataka haki,amani akisisitiza umuhimu wa kutunza amani.
"Kama hujawahi kuishi nje ya Tanzania hautoweza kuelewa maana ya kutunza amani,lakini ukitoka huko utaona umuhimu huo," amesema.

Aidha, amesisitiza umoja kupendana, kuthaminiana ili kuacha alama nzuri duniani na kueleza kwamba kila mtu ni wa muhimu na anapaswa kuchapa kazi.
Akimuelezea hayati Dkt. Magufuli, Askofu Masondole ameelez kwamba kazi nzuri zilizofanywa na Hayati Magufuli ni za Ukombozi na kusisitiza watu kuachana na uchoyo,ubinafsi na ufisadi,kusimama imara kama kielelezo cha kumkumbuka Dkt. John Pombe Magufuli.
Discussion
Reader comments
0 contributions