Serikali ya mkoa wa Tabora imeanza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi, ikiwa ni pamoja na kufungua mashtaka mahakamani na kufuta umiliki wa viwanja.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Kodi ya Pango la Ardhi mkoa wa Tabora, Daniel Bhoke wakati akiwa kwenye ukaguzi, ikiwa ni sehemu ya zoezi linaloendelea la ukusanyaji na uhakiki wa kodi ya pango la ardhi katika Halmashauri zote za mkoa wa Tabora.

Amesema "wadaiwa wote watapatiwa ankara za madai, na endapo watashindwa kulipa ndani ya siku 14 watachukuliwa hatua za kisheria".
Kwa upande wake Afisa Ardhi mteule Manispaa ya Tabora, Damas Mwakimbingo, amewasisitiza wananchi kuwa kila mmiliki wa ardhi anatakiwa kuzingatia masharti ya hatimiliki kwa kulipa kodi kwa wakati.
Discussion
Reader comments
0 contributions