Na Afarah Suleiman, Kiteto - Manyara.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Fadhili Maganya ameipongeza Halmashauri ya Kiteto kwa kusimamia vyema mikopo ya asilimia 10, inayotolewa na Serikali kwa Wanawake ,Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Maganya, ametoa pongezi hizo baada ya kupokea taarifa ya Wilaya ya Kiteto kuhusu utoaji mikopo hiyo, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Manyara.

Aidha, Maganya ameiagiza Halmashauri ya Kiteto kusimamia na kufatikia mfuko wa maendeo ya jamii (TASAF), kuhakikisha fedha zinazotolewa zinawafikia walengwa.
Ziara yake Mkoani Manyara, ilianza Oktoba 2, 2026 na inahitimishwa rasmi hii leo Oktoba 6, 2026 baada ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali katika wilaya zote za mkoa wa Manyara.

Discussion
Reader comments
0 contributions