Skip to main content

KISHAPU WAPOKEA BILIONI 5.2 ZA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

KISHAPU WAPOKEA BILIONI 5.2 ZA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Katika kipindi cha Januari hadi Juni 2026, Wilaya ya Kishapu imepokea  jumla ya Shilingi bilioni 5.2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za afya, elimu, kilimo, umeme, maji, barabara, sekta binafsi, viwanda na uwekezaji huku  hali ya amani, utulivu na usalama,  vikiwa vimeimarishwa ndani ya wilaya hiyo

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Peter Nicholaus Masindi , wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025–2030 kwa kipindi cha Januari-Juni 2026 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Siasa ya CCM Wilaya ya Kishapu, kilichofanyika  katika Ukumbi wa Mikutano wa CCM Wilaya.

DC Masindi amesema kati ya fedha hizo, zaidi ya Shilingi bilioni 3.6 zilitumika katika shughuli na miradi iliyokuwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji lengo likiwa ni kuwahudumia wananchi kuputia miradi hiyo.
Akieleza kuhusu maendeleo ya jamii na uwezeshaji wa wananchi, Mkuu huyo wa Wilaya amesema jumla ya Shilingi milioni 486.3 zilitolewa kama mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, huku wafanyabiashara wadogo 176 wakitambuliwa na kupewa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo.

 Masindi amesema Sekta ya Kilimo Wilaya ilipima sampuli 630 za udongo katika kata 24, kuhamasisha kilimo cha pamba katika ekari 214,232, kusajili wakulima 26,593 kwenye mfumo wa mbolea ya ruzuku na kusambaza tani 2,555 za mbegu za pamba pamoja na viuatilifu kwa wakulima 52,000 katika vijiji 117. Aidha, zana mbalimbali za kilimo zilitolewa ili kuongeza tija kwa wakulima.

Kuhusu umeme, elimu, afya na maji, taarifa hiyo imeeleza kuwa vitongoji 128 vilifanyiwa upembuzi yakinifu na kuanza kuunganishiwa umeme, huku jumla ya vitongoji 428 kati ya 614, sawa na asilimia 69, vikifikikiwa na huduma ya umeme. Kwa upande wa elimu, zaidi ya Shilingi bilioni 1.5 zilipokelewa, huku fedha zikitumika katika mitihani, ujenzi wa miundombinu ya shule na kuboresha mazingira ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Katika sekta ya afya, Wilaya ilipokea zaidi ya Shilingi milioni 872.9, ambapo zaidi ya Shilingi milioni 728.7 zilitumika katika shughuli za maendeleo, ikiwemo afua za lishe, ujenzi wa miundombinu katika vituo vya afya na udhibiti wa TB, HIV na Malaria. Wakati huo huo, huduma ya maji iliongezeka na kufikia kaya 43,277 kutoka kaya 42,401, huku uzalishaji wa maji ukifikia lita milioni 7.9 kwa siku.

Kwa upande wa miundombinu ya barabara, matengenezo ya kawaida na maalum, maeneo korofi pamoja na ujenzi wa makalavati yamefanyika katika barabara zinazounganisha maeneo mbalimbali ikiwemo Mwadui–Lohumbo, Mondo, Sekebugoro, Maganzo, Idukilo, Bunambiyu, Busangwa na Songwa, kwa kutumia Shilingi milioni 456.2 kutoka Mfuko wa Bodi ya Barabara.

Aidha, taarifa hiyo imeonesha hatua zilizopigwa katika viwanda na uwekezaji, ambapo wawekezaji wawili wamekaribishwa, wakiwemo mwekezaji wa kituo cha mafuta na kiwanda cha kusindika alizeti, huku maeneo ya uwekezaji wa viwanda vidogo yakitengwa Isoso na Lubaga.

Baada ya uwasilishaji huo, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benard Werema, alipata nafasi ya kutoa neno la shukrani kwa Mkuu wa Wilaya kwa uwasilishaji mzuri wa taarifa hiyo, huku wajumbe wa kikao wakiipitisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani iliyowasilishwa.

Taarifa hiyo imehitimisha kwa kueleza kuwa Wilaya ya Kishapu imeanza kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2025 kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2026, kwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa vipaumbele vilivyoainishwa katika Ilani hiyo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.