Skip to main content

KISA MAPATO: MADIWANI WAKATWA POSHO SINGIDA

Na Saulo Stephen - Singida .

KISA MAPATO: MADIWANI  WAKATWA POSHO SINGIDA

Na Saulo Stephen - Singida .

Ili kuhakikisha viongozi na watendaji wanawajibika ipasavyo katika kusimamia vyanzo vya mapato, Halmashauri ya Wilaya ya Singida mkoani Singida imekata posho za kila mwezi za madiwani sita baada ya kata wanazoziongoza kushindwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato.

Hatua hiyo imetokana na utekelezaji wa maazimio ya kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Mei mwaka huu, ambapo madiwani walielekezwa kuhakikisha kila kata inafikisha angalau asilimia 50 ya malengo yake ya ukusanyaji wa mapato ifikapo mwisho wa mwaka wa fedha.

Akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani, kilichofanyika Septemba 3, 2026 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Elia Digha, amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya baadhi ya madiwani kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kusimamia ukusanyaji wa mapato katika kata zao.

Digha amesema utekelezaji wa maazimio hayo hautaishia kwa madiwani pekee, bali hatua zaidi zitachukuliwa dhidi ya watendaji wa kata na vijiji watakaobainika kushindwa kutimiza wajibu wao katika kusimamia vyanzo vya mapato.

Amesema lengo la hatua hiyo ni kuhakikisha halmashauri inapata fedha zinazostahili kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo na kuendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.