Na Afarah Suleiman, Babati - Manyara.
Wananchi wa kijiji cha Kiru Six, Wilayani Babati Mkoani Manyara wameishukuru Serikali kwa kuwapatia maji safi na salama kupitia mradi uliotekelezwa na wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijiji Ruwasa.
Wakizungumza katika eneo la mradi huo, Wananchi hao wamesema kwasasa wanapata maji safi na salama na kuiomba serikali kusambaza maji hayo katika maeneo mbalimbali ikiwemo Shuleni na Hospitali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Babati, BAWASA, Idd Msuya na Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini vijiji RUWASA, James Kionaumela wamesema kwa sasa hali ya upatikanaji wa Maji katika kijiji hicho unaridhishi na kuhaidi kuendelea kufikisha huduma kwa Wananchi.



Discussion
Reader comments
0 contributions