Skip to main content

KIKWETE KUSIKILIZA, KUTATUA KERO ZA WANANCHI TABORA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Jakaya Kikwete yupo mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ya kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma za umma.

KIKWETE KUSIKILIZA, KUTATUA KERO ZA WANANCHI TABORA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Jakaya Kikwete yupo mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ya kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma za umma. 

Akiwasili mkoani humo amepokelewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora Upendo Wella na Katibu Tawala wa Mkoa, Dkt. John Rogath Mboya.

Katika ziara hiyo, waziri Kikwete amekagua miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.223 katika wilaya za Igunga na Nzega, ikiwemo Kituo cha Afya Kining'inila, Daraja la Nyandekwa, nyumba za Wakuu wa Idara na miundombinu ya Shule ya Sekondari Puge huku akipongeza wananchi na watendaji wa serikali kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo na kuwataka kuendelea kushirikiana katika kuharakisha maendeleo. 

Akizungumza na watumishi wa umma, Waziri Kikwete amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kulinda haki na maslahi yao kwa kuhakikisha madai ya uhamisho, upandishaji wa vyeo na stahiki nyingine yanashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni. 

Aidha, amekemea vitendo vya kuchelewesha au kunyima watumishi haki zao na kusisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kutekeleza ahadi zake kwa wananchi huku ikihimiza wananchi kulinda amani, kupuuza uchochezi na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo. 

Amesema "Tekelezeni wajibu wenu. Wale mliopewa dhamana ya kuhakikisha ustawi wa maisha ya wananchi unakwenda vizuri, timizeni wajibu huo kwa uaminifu. Hatupendi kusikia wananchi wetu wanalalamika."

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.