Skip to main content

KIJANA JELA MIAKA 35 KWA KUBAKA, KUMPA MIMBA MWANAFUNZI

Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imemhukumu Alphonce Meshack Alphonce (19) kifungo cha jumla ya miaka 35 jela kwa makosa mawili ya ubakaji na kumpa mimba mwanafunzi.

KIJANA JELA MIAKA 35  KWA KUBAKA, KUMPA MIMBA MWANAFUNZI
Studio Narration JAMBO FM

KIJANA JELA MIAKA 35 KWA KUBAKA, KUMPA MIMBA MWANAFUNZI

0:00 --:--

Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoani  Katavi imemhukumu Alphonce Meshack Alphonce (19) kifungo cha jumla ya miaka 35 jela kwa makosa mawili ya ubakaji na kumpa mimba mwanafunzi.

Mahakama ilimkuta mshitakiwa na hatia ya kutenda makosa hayo katika nyakati tofauti kati ya Februari 2026 hadi Julai 2026 uko mtaa wa Nguvumali, kata ya Mwamkulu Tarafa ya Misunkumilo Wilayani Mpanda Mkoani Katavi ambapo alidaiwa kufanya tendo la ndoa kinyume cha sheria na Mwanafunzi huyo.

Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka ameeleza mahakama hiyo, kuwa kosa la kwanza la ubakaji lilikua kinyume na kifungu cha 130(1) na (2)(e) pamoja na kifungu cha 131(1) cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code) Sura ya 16 kwa sababu mwanafunzi mwenye miaka 14 anahesabiwa kisheria kuwa ni mtoto asiye na uwezo wa kutoa idhini ya kimapenzi.

Kosa la pili ni la kumpa Mwanafunzi mimba ilitajwa kuwa kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 60A(3) cha Sheria ya Elimu (Education Act) Namba 353 (marejeo ya mwaka 2002) ambayo inakataza kumhusisha mwanafunzi katika mahusiano ya kimapenzi au kumsababishia ujauzito.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili katika shauri hilo, Mahakama ilimkuta mshitakiwa na hatia katika makosa yote mawili ambapo katika kosa la kwanza la ubakaji mahakama ili muhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani na katika kosa la pili la kumpa Mwanafunzi mimba mahakama ili muhukumu kifungo cha miaka 5 gerezani ambapo adhabu zote zitatekelezwa kwa pamoja.

Shauri hilo lilisikilizwa mbele ya hakimu mfawidhi mwandamizi Mhe. Rebeca Mwalusako na hukumu kutolewa Octoba 22, 2026 ambapo alitaja hukumu hiyo ni fundisho kwa jamii na mwendelezo wa hatua za kisheria zinazochukuliwa dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi na watoto.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.