Skip to main content

KIJANA ALIYEUWA WATATU KATAVI AHUKUMIWA KUNYONGWA

Na Daniel Gahu - Katavi.

KIJANA ALIYEUWA WATATU KATAVI AHUKUMIWA KUNYONGWA

Na Daniel Gahu - Katavi.

Mahakama kuu ya Mkoa wa Katavi imemuhukumu Shija Charles mwenye umri wa miaka (26), Kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya mauaji ya kukusudia ya watu watatu wa familia moja huko katika kitongoji cha Busongola, kata ya Bulamata, Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi.

Akisoma hukumu hiyo Machi 23, 2026, Hakimu Mfawidhi Sumary Gway amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 5, 2024 ambapo aliwaua Monica Kingwa (24), Siwema Shija (2) na Yanga Shija mwenye umri wa miezi 8 kwa kuwashambulia kwa kitu chenye ncha kali (panga )sehemu mbalimbali za miili yao, tukio linalodaiwa kuhusishwa na imani za kishirikina za kutafuta utajiri.

Amesema, mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022 na kueleza adhabu hiyo imetolewa ili iwe fundisho kwa washitakiwa na jamii katika kukomesha vitendo vya kikatili.

Awali Kesi hiyo ilifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Juni 14, 2024 na hukumu kutolewa Machi 23, 2026 ambapo Hakimu Mfawidhi amebainisha kuwa mahakama imejiridhisha pasiposhaka na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri na umetosha kumtia hatiani mtuhumiwa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.