Na Clavery Christian, Bukoba - Kagera.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Kenani Raban Kihongosi ameanza rasmi ziara yake ya kikazi mkoani Kagera kwa kukagua utekelezaji wa miradi ya Soko Jipya la Kisasa pamoja na Stendi ya Mabasi katika Manispaa ya Bukoba.
Akikagua ujenzi huo, Mwenezi Kenani ameridhishwa na kusema kuwa ujenzi unaendana na thamani ya fedha iliyowekezwa jambo linaloonesha kwa vitendo matumizi sahihi ya rasilimali za umma na usimamizi mzuri wa mradi huo mkubwa.

Ujenzi wa soko kuu la Bukoba unagharimu jumla ya Tsh Bilioni 18.9 fedha zilizotokana na mkopo wa Benki ya Dunia ambapo Ndugu Kenani akiridhishwa na matumizi ya fedha na utekelezwaji wa mradi huo.
Mwenezi Kenani amezitaka Mamlaka za Wilaya kuweka utaratibu wa haki kwa kutoa kipaumbele kwa wafanyabiashara waliokuwepo awali kupewa nafasi katika soko hilo mara baada ya kukamilika kwake hatua itakayosaidia kuepusha malalamiko yasiyo ya lazima.

Ujenzi wa soko hilo litakalokuwa na jumla ya Vizimba 1,848, Maduka 234 (yakiwema 132 ya chini na 102 ya juu), Huduma mbalimbali za kijamii, Ofisi 4, Mabucha 12, Pamoja na Maegesho ya magari madogo 47 na makubwa 32 unatajawa kuwa utaboresha mazingira ya biashara kwa wakazi wa Bukoba na kuchochea ukuaji wa uchumi.


Discussion
Reader comments
0 contributions