Na Ibrahim Rojala, Chato - Geita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chato, Mandia Kihiyo ameongoza Kikao cha Baraza la Biashara cha Halmashauri ya Wilaya ya Chato kilichofanyika Juni 30, 2026 kujadili shughuli za kiuchumi katika ukumbi wa Stendi ya Kahumo kilichowakutanisha wafanyabiashara, wakuu wa sekta za umma na sekta binafsi.
Kupitia kikao hicho kilichoketi mijadala ilijikita katika kuibua fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta za kilimo cha kisasa kwa njia ya umwagiliani na Green House, uvuvi, ufugaji, biashara na madini, uanzishaji wa viwanda vya kusindika mazao, uvuvi wa kisasa, ufugaji wa kisasa, biashara za usafirishaji.

Kihiyo amesisitiza matumizi ya mifumo ya kidijitali kwa wafanyabiashara kujisajili na kutumia teknolojia za kisasa, ili kuongeza wigo wa uzalishaji na masoko ya bidhaa na huduma zao pamoja na kuandaa kikao cha Wilaya kitakachoinua fursa mbalimbali zinazopatikana Wilayani humo.
Aidha, aliwahamasisha wananchi na wawekezaji kutumia fursa zilizopo, ikiwemo vibanda vya biashara katika kituo cha Mabasi Kahumo vinavyopatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= tu kwa mwezi kwa vibanda vya kawaida na ushiriki wao katika nyama choma inayofanyika kila jumamosi katika kituo hicho cha mabasi.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wilaya ya Chato, Jovin Mwarabu ameeleza kwamba wamekubaliana kuzitangaza fursa zilizopo wilayani Chato na kuelezea taratibu za uwekezaji kupitia fursa hizo kwa kuandaa kitini kitakachokuwa na maelezo muhimu kuhusiana na uwekezaji na kusisitiza wafanyabiashara kuendelea kutumia mifumo mbalimbali ya serikali kama vile TAUSI, ambayo baadhi yake ina fursa za kibiashara.
“Halmashauri ina fursa nyingi sasa tunakuwa tunalalamika kuwa fursa hazipo lakini inaonekana kuna baadhi tu ya upungufu wa elimu,basi tumesisitizana hayo,baraza limekwenda vizuri na tumemaliza kwa mafanikio makubwa,” ameeleza Mwarabu.

Hatq hivyo, amewataka Wafanyabiashara na wawekezaji kuchangamkia fursa zilizopo ndani ya wilaya hiyo, ikiwa ni pamoja na kilimo, utalii, ufugaji, uvuvi na sekta ya madini.

Discussion
Reader comments
0 contributions