Na Tryphone Odace, Kibondo - Kigoma.
Wananchi wa Vijiji vya Kumuhasha, Kumrungu na Kumbanga Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma, wamesema kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha afya Murungu, kutatatua changamoto za kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya na wakati mwingine wanawake kujifungulia njiani na kusabaisha vifo.
Wakizungumza na Jambo Media, baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo akiwemo Martha Jorodan na Aisha Maneno wamesema, changamoto ya kupata huduma za afya za uhakika ziliwalazimu kwenda vijiji jirani au Hospitali ya Wilaya ya Kibondo iliyopo umbali wa zaidi ya kilimeta 10 kutoka katika makazi yao.
Stamili Omary mkazi wa kijiji cha Kumuhasha alisema, Serikali imeelekea kumaliza changamoto za muda mrefu ikiwemo vifo vya baadhi ya wagonjwa kutokana na umbali mrefu wa kuzifikia huduma za afya kutoka vilipo vijiji hivyo.

Aidha wananchi hao walieleza kuwa kwa sasa wanaona wakienda kuepukana na gharama kubwa za usafiri kupeleka wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ambapo walilazimika kutumia zaidi ya shilingi elfu 25 kumsafirisha mgonjwa kutokana na umbali lakini ukosefu wa miundombinu bora ya usafirishaji.
Ujenzi wa kituo hicho umegharimu kiasi cha shilingi 252,700,000 ambapo shilingi 250,000,000 ikiwa ni fedha kutoka serikali kuu, 1,250,000 kutoka halmashauri huku michango ya wananchi ikiwa 1,450,000, ukihusisha jengo la wagonjwa wa nje na kichoma taka.
Hata hivyo wananchi hao wamesema kwa kuona adhaa na usumbuu waliokuwa wanaupata wa kufuata matibabu mbali kiliwasukuma kutoa michango yao ili kusaidia ujenzi wa kituo hicho kuanza kujengwa na sasa kwao wanaona ni mwanga na mwanzo wa kufanya shughuli za maendeleo bila kutumia muda mwingi katika suala la kutafuta huduma za afya.

Haya yote yalijili wakati mwenge wa uhuru 2026 ulipowasili katika Kijiji cha Kumhasha kwa ajili ya kuzindua ujenzi wa kituo cha afya Murungu ambacho kinakwenda kufungua fursa za upatikanaji huduma za afya katika vijiji vya Kumuhasha, Kumrungu na Kumbanga.
Naye kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2026 Wazo Mwangonda aliupongenzi uongozi wa vijiji hivyo na viongozi wa halmashauri ya Wilaya Kibondo kwa kusimamia vyema mradi huo na kukamilika kwa ubora nkubwa katika hatua hiyo ya awali.
Mwang'onda alisema Serikali hairidhishwi kuona wananchi wake wanapata huduma za afya mbali na maeneo ya makazi na kuamua kusogeza huduma za afya jirani na makazi ya wananchi.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, kata ya Murungu iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma ina jumla ya wakazi 84,400 na hii inaifanya kata ya Murungu kuwa ndiyo eneo lenye idadi kubwa zaidi ya watu kuliko kata zote zilizopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya Kibondo Mkoani Kigoma na kuifanya kuwa na uhitaji mkubwa wa kituo cha afya kitakachokidhi mahitaji ya wananchi wa kata hiyo na maeneo Jirani katika suala la huduma za afya.
Aidha mwenge wa uhuru umehitimisha mbio zake katika Wilaya Kibondo leo September 9 umepokelewa katika halmashauri ya Wilaya Kasulu ambapo utakagua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo.
Discussion
Reader comments
0 contributions