Skip to main content

KIARATU: MTAMAA TUMIENI FURSA ZA SERIKALI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Wananchi wa Kata ya Mtamaa Manispaa ya Singida, Mkoani Singida wamehimizwa kutambua na kutumia kikamilifu fursa mbalimbali zinazotengenezwa na kuwezeshwa na Serikali, kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao.

KIARATU: MTAMAA TUMIENI FURSA ZA SERIKALI KUJIKWAMUA KIUCHUMI
Studio Narration JAMBO FM

KIARATU: MTAMAA TUMIENI FURSA ZA SERIKALI KUJIKWAMUA KIUCHUM...

0:00 --:--

Wananchi wa Kata ya Mtamaa Manispaa ya Singida, Mkoani Singida wamehimizwa kutambua na kutumia kikamilifu fursa mbalimbali zinazotengenezwa na kuwezeshwa na Serikali, kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Yagi Kiaratu, ametoa rai hiyo katika ziara yake kwenye Kata ya Mtamaa, ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuwa karibu na wananchi, kusikiliza maoni yao pamoja na kufahamu changamoto zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini,Yagi Kiaratu akiongea na wananchi wa kata ya Mtamaa Jimboni kwake.

Amesisitiza kuwa uwepo wa fursa pekee hautoshi, bali wananchi wanapaswa kuzitambua, kuzichangamkia na kuzitumia kwa vitendo ili ziweze kuleta matokeo chanya katika familia zao na jamii kwa ujumla.

Sehemu ya Wananchi wa Mtamaa Wakiwa kwenye Mkutano wa Ziara ya Mbunge wa Singida Mjini Yagi Kiaratu.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha mawasiliano kati ya wananchi na viongozi, huku Kiaratu akiendelea kusikiliza maoni na changamoto za wananchi kwa ajili ya kufahamu maeneo yanayohitaji ufuatiliaji na hatua zaidi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.