Skip to main content

KIARATU ASISITIZA MALEZI BORA, MAADILI KWA VIJANA

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Yagi Kiaratu, amesisitiza umuhimu wa malezi bora na ujenzi wa maadili kwa vijana, akieleza kuwa maadili mema ni msingi wa kujenga jamii imara na yenye maendeleo.

KIARATU ASISITIZA MALEZI BORA, MAADILI KWA VIJANA
Studio Narration JAMBO FM

KIARATU ASISITIZA MALEZI BORA, MAADILI KWA VIJANA

0:00 --:--

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Yagi Kiaratu, amesisitiza umuhimu wa malezi bora na ujenzi wa maadili kwa vijana, akieleza kuwa maadili mema ni msingi wa kujenga jamii imara na yenye maendeleo.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kata ya Mwankoko, Kiaratu amewataka wazazi kuwa karibu na vijana wao, kuwasikiliza, kuwaongoza na kuwajenga katika misingi ya heshima, nidhamu na uwajibikaji.

Aidha, amewahimiza vijana kuheshimu malezi, kutumia fursa zilizopo na kujenga maisha yao kwa bidii, nidhamu na uwajibikaji, akisisitiza kuwa mafanikio ya kizazi kijacho yanahitaji msingi imara wa maadili.

Kiaratu amesema ujenzi wa kizazi chenye maadili unaanzia nyumbani, huku akitoa wito kwa wazazi, vijana na jamii kwa ujumla kushirikiana katika kulinda na kuimarisha maadili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.