Skip to main content

KATAVI YAWEKA MIKAKATI KUDHIBITI EBOLA

Na Daniel Gahu - Katavi.

KATAVI YAWEKA MIKAKATI KUDHIBITI EBOLA

Na Daniel Gahu - Katavi.

Serikali ya Mkoa wa Katavi imewaagiza viongozi katika ngazi zote mkoani hapa kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola ili waweze kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo hatari.

Maagizo hayo yametolewa wakati wa kikao cha kamati ya Usimamizi wa Afya ya Msingi Mkoa wa Katavi kilichoketi kwa lengo la kuweka mikakati ya kuongeza utayari wa kudhibiti ugonjwa wa Ebola iwapo utatokea.

“Wananchi wasipuuze taarifa na elimu inayotolewa kuhusu ugonjwa wa Ebola, kwani elimu hiyo ni muhimu katika kuchukua tahadhari na kujikinga dhidi ya ugonjwa huo”.

Aidha imesisitiza kuwa hatua zote za upimaji wa afya katika maeneo mbalimbali ya mkoa zinapaswa kuendelea kufanyika kwa ufanisi mkubwa, huku ikiwataka wananchi kutopuuzia taarifa na elimu inayotolewa kuhusu ugonjwa wa Ebola.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Jonathan Budenu amesema kuwa mkoa umeendelea kuchukua hatua mbalimbali za tahadhari na maandalizi ili kuhakikisha mfumo wa huduma za afya unakuwa tayari kukabiliana na ugonjwa huo hatari.

"Wastani wa upatikanaji wa dawa, vifaa tiba pamoja na vifaa kinga kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa wa Ebola umefikia asilimia 35.83 huku juhudi zaidi zinaendelea kuhakikisha mahitaji muhimu yanapatikana kwa kiwango cha kuridhisha," amesema Dkt Budenu.

Ameongeza kuwa wataalam wa afya wameendelea kujengewa uwezo kuhusu namna ya kutoa huduma na matibabu kwa wagonjwa wa Ebola pamoja na mbinu za kujikinga wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Ametaja baadhi ya afua zilizotekelezwa kuwa ni pamoja na kuendesha kikao cha dharura cha Timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya ya Mkoa (RHMT), kuhakiki Mpango wa Mkoa wa Kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola (Ebola Contingency Plan), pamoja na kuimarisha ufuatiliaji wa wasafiri katika maeneo ya kuingilia mkoani (Points of Entry - POE).

Afua nyingine ni kuainisha maeneo ya kutenga matibabu ya wagonjwa wa Ebola (Isolation and Treatment Centers) pamoja na kufanya tathmini ya dawa, vifaa tiba na vifaa kinga kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa wa Ebola.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.