Skip to main content

KATAVI: RAS MSOVERA ATAKA HOJA ZA UKAGUZI ZIPATIWE UFUMBUZI MAPEMA

Na Daniel Gahu - Katavi.

KATAVI: RAS MSOVERA ATAKA HOJA ZA UKAGUZI ZIPATIWE UFUMBUZI MAPEMA

Na Daniel Gahu - Katavi.

Katibu Tawala Mkoa wa Katavi, Albert Msovela amezitaka halmashauri za wilaya mkoani Katavi kuendelea kupunguza hoja za ukaguzi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya Serikali, huku akisisitiza kuwa hoja zilizopo zipatiwe ufumbuzi bila kusubiri ujio wa wakaguzi wa nje wa hesabu za Serikali.

Akizungumza katika baraza maalumu la kupitia hoja za Mkaguzi wa Nje wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa hesabu 2024/2025, Juni 29,2026 amesema licha ya idadi ya hoja za ukaguzi kuendelea kupungua, bado kuna kazi kubwa ya kuimarisha ufuatiliaji wa sheria, kanuni na miongozo ili kuondoa mapungufu yanayojitokeza.

"Hoja zimeendelea kupungua, lakini bado tunapaswa kuongeza juhudi katika kufuata sheria, kanuni na miongozo ya Serikali. Hoja zilizopo zinaweza kutafutiwa ufumbuzi bila kusubiri wakaguzi wa nje," amesema Bw. Msovela.

Aidha, amewataka wataalamu kushirikiana katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kufuata maagizo ya Kamati ya Fedha, kujitathmini katika utendaji wao na kufanya kazi kwa ufanisi ili kuepusha hoja zisizo na mashiko ambazo zinaweza kuathiri utekelezaji wa shughuli za Serikali.

"Kila mtaalamu awajibike ipasavyo, afanye kazi kwa ufanisi na ahakikishe hatoi nafasi ya kujitokeza kwa hoja zisizo na mashiko ambazo zinaweza kuikwamisha Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo," amesisitiza.

Katika hatua nyingine,ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kutoa fedha za maendeleo, ambapo zaidi ya shilingi bilioni 41 zimeelekezwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali tangu kuanza kwa awamu hiyo ya Serikali.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.