Skip to main content

KATAMBI AWAONYA WANAOTOA KAULI ZA KICHOCHEZI MITANDAONI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amewaasa watu wanaotoa kauli za kichochezi katika mitandao ya kijamii, majukwaa ya kisiasa na maeneo mbalimbali ambapo kauli hizo za kibaguzi na kichochezi zinahusu Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Viongozi mbalimbali wa serikali au wa dini.

Waziri Katambi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waumini wa Msikiti wa Mukadam uliopo Kata ya Chang’ombe iliyopo wilaya ya Dodoma Mjini, ambapo kumefanyika Mashindano ya Quran na Harambee ya Ujenzi wa Msikiti huo.

Amesema, “Taifa hili limejengwa kwa maumivu makubwa ya waasisi, limejengwa kwa jasho na hata damu ilipobidi ili Taifa Tanzania liwepo, nitumie fursa hii kuwaomba sana na kuwaasa wale wote ambao wanatumia majukwaa ya kisiasa kuchonganisha wananchi, kuwajaza chuki, kuchochea lakini pia kuhamasisha kufanya uhalifu na wanaounda magenge ya uhalifu yanayolenga kuharibu taifa letu, niwasihi na kuwaomba waache mara moja."

Katambi ameongeza kuwa, “tutarudi nyuma kimaendeleo, tutashindwa kuswali, tutashindwa kwenda kanisani, tutashindwa kufanya kazi za kiuchumi, tutashindwa kujenga nchi yetu, utashindwa kujenga uchumi wa mtu mmoja mmoja tuwakanye na kuwaelekeza vijana wetu wakaishi mwenendo mwema na uzalendo kwa taifa lao."

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.