Skip to main content

KATAMBI AKEMEA SIASA ZA CHUKI, ATOA HAKIKISHO LA USALAMA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amewahakikishia amani na utulivu wananchi wa Tanzania huku akiwataka kuendelea na shughuli za kiuchumi na maendeleo hata katika tarehe inayotajwa mitandaoni kuwa kutakua na maandamano nchi nzima.

Katambi pia amesema Vyombo vya Usalama vimejipanga kulinda amani ya nchi hii ambapo pia ameziomba mamlaka husika kupitia Wakurugenzi wa Miji na Mikoa kusimamia miundombinu ya barabara ili huduma za Uokoaji na zimamoto ziweze kufika katika eneo la tukio.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi.

Ameyasema hayo wakati wa Hafla ya
kufunga Mafunzo ya Awali, Kozi Na.6/2026 katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Chogo, kilichopo wilayani Handeni mkoani Tanga, wakati askari 1,000 wakihitimu mafunzo hayo.

Awali akizungumza katika Hafla hiyo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suruhu Hassan kwa kutoa kibali hicho cha kuajiri askari hao waliohitimu, huku akithibitisha taratibu zote za ajira kukamilika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.