Skip to main content

KASULU: MIL. 100 KUTUMIKA ULIPAJI FIDIA WALIOPISHA ENEO LA UJENZI SHULE MPYA YA MSINGI

Zaidi ya shilingi milioni 100 zinahitajika kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi wa Kata ya Mwilamvya, Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma, waliopisha maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya msingi.

KASULU: MIL. 100 KUTUMIKA ULIPAJI FIDIA WALIOPISHA ENEO LA UJENZI SHULE MPYA  YA MSINGI
Studio Narration JAMBO FM

KASULU: MIL. 100 KUTUMIKA ULIPAJI FIDIA WALIOPISHA ENEO LA U...

0:00 --:--

Zaidi ya shilingi milioni 100 zinahitajika kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi wa Kata ya Mwilamvya, Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma, waliopisha maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya msingi.

Akizungumza kuhusu suala hilo, Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Mwilamvya, Iddy Emmanuel, amesema mchakato wa kufanya uthamini wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo umekamilika.

Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Mwilamvya, Iddy Emmanuel

Amesema hatua inayofuata ni kufanya mazungumzo na wananchi kuhusu namna ya kuchangia fedha zitakazosaidia kufanikisha ujenzi wa shule hiyo.

Kwa mujibu wa Emmanuel, ongezeko la idadi ya wanafunzi katika kata hiyo limeongeza uhitaji wa kuwa na shule nyingine ya msingi, kwani kwa sasa kata hiyo ina shule moja tu ya msingi ya serikali.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mwilamvya, Emmanuel Gamuye, amewahimiza wananchi kuweka kipaumbele katika kuchangia shughuli za maendeleo ili kuharakisha utekelezaji wa miradi inayolenga kuboresha huduma katika kata hiyo.

Diwani wa Kata ya Mwilamvya Halmashauri ya Mji wa Kasul, Emmanuel Gamuye

Gamuye ameeleza kuwa wananchi wanapaswa kuelekeza nguvu na rasilimali zaidi katika shughuli za maendeleo badala ya kutumia sehemu kubwa ya rasilimali zao katika sherehe za harusi.

Naye, baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwilamvya wamesema ongezeko la idadi ya watoto limekuwa miongoni mwa sababu zilizowasukuma kushirikiana na viongozi kuanzisha mchakato wa ujenzi wa shule mpya ya msingi.

Pichani ni baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwilamvya

Wamesema ujenzi wa shule hiyo unalenga kukidhi mahitaji ya elimu yanayotokana na ongezeko la watoto katika kata hiyo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.