Skip to main content

KASANGEZI WAASHIMISHA SIMBA DAY KWA KUFANYA USAFI ZAHANATI

Mashabiki wa Klabu ya Soka ya Simba kutoka Kijiji cha Kasangezi, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, wameadhimisha Siku ya Simba Day kwa kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira katika Zahanati ya Kasangezi.

KASANGEZI WAASHIMISHA SIMBA DAY KWA KUFANYA USAFI ZAHANATI

Mashabiki wa Klabu ya Soka ya Simba kutoka Kijiji cha Kasangezi, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, wameadhimisha Siku ya Simba Day kwa kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira katika Zahanati ya Kasangezi.

Zoezi hilo ni sehemu ya shughuli za kijamii zilizoandaliwa na mashabiki hao katika kuadhimisha Simba Day, huku likilenga kuchangia juhudi za jamii katika kuhakikisha mazingira ya maeneo ya kutolea huduma za afya yanakuwa safi na salama.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mratibu wa Sherehe za Simba Day na Siku ya Mwananchi kutoka Kijiji cha Kasangezi, Rukata Elias, amesema maadhimisho hayo yamekuwa fursa ya kuwaunganisha mashabiki wa Simba na jamii katika kutekeleza shughuli mbalimbali zenye manufaa kwa wananchi.

Amesema uamuzi wa kufanya usafi katika zahanati hiyo umetokana na umuhimu wa kuwa na mazingira safi katika vituo vya huduma za afya, ili kulinda afya na ustawi wa wagonjwa pamoja na watumishi.

“Tumeamua kutumia maadhimisho haya kufanya jambo lenye manufaa kwa jamii yetu. Zahanati ni eneo muhimu, hivyo ni wajibu wetu kushirikiana kuhakikisha linakuwa safi na salama,” amesema Elias.

Kwa upande wao, baadhi ya mashabiki wa Simba walioshiriki katika zoezi hilo wamesema wameamua kuadhimisha Simba Day kwa vitendo kwa kushiriki shughuli zinazogusa moja kwa moja maisha ya wananchi.

Wamesema hatua hiyo inaonesha kuwa michezo inaweza kuwa chachu ya mshikamano na maendeleo ya jamii, na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana katika kutunza usafi wa mazingira, hususan katika maeneo ya huduma za kijamii.

Mashabiki hao pia wamewataka wadau wengine wa michezo kutumia matukio mbalimbali ya michezo kama fursa ya kuhamasisha shughuli za kijamii na kuchangia maendeleo ya maeneo wanayoishi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.