Skip to main content

KAMPENI UTEKELEZAJI MALEZI CHANYA, MAADILI KWA WATOTO TARIME WAENDELEA

Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara imesema inaendelea kutekeleza kampeni ya malezi chanya na maadili kwa watoto, huku ikitoa wito kwa wazazi na walezi kushiriki kikamilifu katika kuwajenga watoto katika misingi bora ya maadili.

KAMPENI UTEKELEZAJI MALEZI CHANYA, MAADILI KWA WATOTO TARIME WAENDELEA

Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara imesema inaendelea kutekeleza kampeni ya malezi chanya na maadili kwa watoto, huku ikitoa wito kwa wazazi na walezi kushiriki kikamilifu katika kuwajenga watoto katika misingi bora ya maadili.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Juni,16 2026 yaliyofanyika mjini Tarime, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Vitus Gwanko, amesema kampeni hiyo inayotekelezwa kuanzia Juni 16 hadi Juni 30 mwaka huu inalenga kuimarisha malezi bora ya watoto na kukabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili katika jamii.

Kwa upande wake, Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto wilayani Tarime, Inspekta Amina Hozza, ameitaka jamii kuachana na mila potofu na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, ikiwemo ukeketaji, ndoa za utotoni pamoja na kuwafanyisha watoto kazi zinazokiuka sheria za nchi.

Aidha, washiriki mbalimbali katika maadhimisho hayo akiwemo Afisa Maendeleo ya Jamii, Ghati Ngogo, pamoja na viongozi wa dini wamesisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kushiriki kikamilifu katika malezi ya watoto ili kuwajengea maadili mema na kuwasaidia kufikia ndoto zao.

Wakizungumza katika maadhimisho hayo,baadhi ya wazazi wamesema wataendelea kushirikiana na serikali pamoja na wadau mbalimbali katika kuhakikisha watoto wanapata malezi bora yatakayowasaidia kuwa raia wema na wenye mchango chanya kwa taifa.

Maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Mtoto wa Afrika yamefanyika chini ya kauli mbiu isemayo, “Mtoto ni Malezi, Msingi wa Familia Bora kwa Taifa Imara.”

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.