Skip to main content

KAMPENI “ONGEA NA KAMANDA” YASIKILIZA KERO ZA WANANCHI TABORA

Wananchi wa Kata ya Itetemia mkoani Tabora wametumia kampeni ya “Ongea na Kamanda” kufikisha kero na changamoto mbalimbali za kiusalama, zikiwemo ukatili, ubakaji, migogoro ya ardhi na ufugaji holela.

KAMPENI “ONGEA NA KAMANDA” YASIKILIZA KERO ZA WANANCHI TABORA
Studio Narration JAMBO FM

KAMPENI “ONGEA NA KAMANDA” YASIKILIZA KERO ZA WANANCHI TABOR...

0:00 --:--

Wananchi wa Kata ya Itetemia mkoani Tabora wametumia kampeni ya “Ongea na Kamanda” kufikisha kero na changamoto mbalimbali za kiusalama, zikiwemo ukatili, ubakaji, migogoro ya ardhi na ufugaji holela.

Kampeni hiyo inayoendeshwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora inalenga kufika katika kata zote 206 za mkoa huo, kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana nao katika kuzitafutia ufumbuzi.

Kamishna Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Tabora, Twaha Lulengelule, amesema Jeshi la Polisi litazifanyia kazi hoja zilizowasilishwa na wananchi kwa mujibu wa sheria.

Amesema wananchi wanapaswa kuendelea kutoa taarifa na kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kukabiliana na vitendo vinavyohatarisha usalama katika maeneo yao.

Kampeni hiyo itaendelea katika kata mbalimbali za Mkoa wa Tabora, huku wananchi wakipewa nafasi ya kueleza changamoto zinazowakabili na kupata ufafanuzi kutoka kwa Jeshi la Polisi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.