Skip to main content

KAMATI YA FEDHA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KISHAPU

Na Eunice Kanumba –Shinyanga.

KAMATI YA FEDHA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KISHAPU

Na Eunice Kanumba –Shinyanga.

Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imefanya ziara maalum ya kukagua miradi 7 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 1, 278,000,000.

Ziara ambayo imeongozwa  na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Enock Reuben ambapo wajumbe wa kamati hiyo wamtembelea ili kujionea hali halisi ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ile  inayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi, ikiwemo miradi ya afya, umeme wa jua, ujenzi wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo kwenye baadhi ya zahanati na maegesho ya magari  katika mnada wa Mhunze.

Mingine ni ujenzi wa nyumba mpya ya Mkurugenzi Mtendaji, ujenzi wa vichomea taka katika zahanati, pamoja na maendeleo ya kikundi cha Vijana na Wanawake waliopewa mikopo ya asilimia 10 wa Halmashauri hiyo.

Kwa mujibu wa kamati hiyo, lengo kuu la ziara lilikuwa ni kufuatilia kwa karibu matumizi ya fedha za miradi, kutathmini hatua za utekelezaji, pamoja na kubaini changamoto zinazoweza kukwamisha ukamilishaji wa miradi hiyo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, makamu mwenyekiti wa halimashauri ya wilaya ya Kishapu Enock  Reuben amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kila shilingi ya umma inaleta thamani halisi kwa wananchi (value for money), huku akiwataka watendaji kusimamia miradi kwa weledi na uwajibikaji mkubwa.

Katika hatua nyingine kamati hiyo imetoa  maelekezo na ushauri muhimu kwa watendaji kufanya   usimamizi makini wa fedha za miradi, kwa kuzingatia  viwango vya ubora wa ujenzi, pamoja na  kukamilika kwa miradi ndani ya muda uliopangwa pamoja na utatuzi wa changamoto kwa wakati.

Nao baadhi ya wananchi katika halimashauri hiyo wameipongeza kamati hiyo kwa hicho ilichokifanya kwani kimeonyesha  dhamira ya dhati ya viongozi wa Kishapu katika kusimamia maendeleo na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ina nafasi muhimu katika kusukuma maendeleo ya wilaya. Kupitia ziara kama hizo, kwa lengo  la kuhakikisha uwajibikaji unaimarika, fedha zinatumika ipasavyo, na miradi inatekelezwa kwa ufanisi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.