Skip to main content

KAMA NI KWELI WAKUBWA 'WALITUPIGA KAMBA' TUWAOMBE KIKAO

Mambo ni mengi Duniani! Ndugu yangu hivi unakumbuka hata wewe? bila shaka ulishawahi kusikia hadithi nyingi ambazo uliamini ni za kweli lakini kiuhalisia tulidanganywa tukiwa wadogo .

KAMA NI KWELI WAKUBWA 'WALITUPIGA KAMBA' TUWAOMBE KIKAO
Studio Narration JAMBO FM

KAMA NI KWELI WAKUBWA 'WALITUPIGA KAMBA' TUWAOMBE KIKAO

0:00 --:--

Mambo ni mengi Duniani! Ndugu yangu hivi unakumbuka hata wewe? bila shaka ulishawahi kusikia hadithi nyingi ambazo uliamini ni za kweli lakini kiuhalisia tulidanganywa tukiwa wadogo .

Inachinjwa Ng'ombe kifamilia familia si unajua tena shughuli zetu katika jamii, halafu linatoka tamko eti vya ndani watoto hawalagi.

Wahenga walitupiga sana, yaani inatafutwa tu sababu ili mradi wafaidi wao kwanza halafu nyie mnatulizwa, hii sio poa.

Hapa nakusogezea baadhi ya hadithi tulizowahi kusikia ambazo zilituqcha mdomo wazi na kutupa vitisho lakini baadaye tukaja ng'amua kuwa hazina ukweli.

1. MLUZI.

Tuliambiwa ni marufuku, yaani uipige mmluzi nyakati za usiku eti hiyo inakuwa unaita majini / nyoka.

Lakini kiuhalisia hapo hakuna kitu, maana mluzi ni hewa tu na Majini hayaishi kwa miluzi.

2. MBEGU.

Hapa watu wa Kyela kule mpaka Ipinda watanisoma haraka, sio wao tu hata sehemu yeyote ambayo inalimwa zao la Kakao.

Wakubwa walitupanga wakisema tusimeze mbegu za Kakao, sasa huku mikoa mingine nao wakaiga na kwenda mbali zaidi eti kwa sababu hamna Kakao, nao waka 'copy' eti tusimeze mbegu ya chungwa/ embe maana tutaota mti tumboni/ Kichwani.

Tumelia sana kwa hili! lakini ukweli ni kwamba Asidi ya tumboni inaua kila mbegu na hakuna mti unaweza kuota tumboni na hata mti kuota kichwani ni vitisho tu wanangu.

3. KUCHA / NYWELE.

Hao hao wahenga wetu, kwa mara nyingine walidai kwamba ukikata kucha/nywele nyakati za usiku, basi utapata mkosi au mapepo.

Hii ilitengenezwa zamani kwa sababu hakukuwa na umeme - watu walikata kucha au kunyoa bila kujali nyakati, lakini haikuwa laana ni mmabo yao tu, yaani ukimuhoji sana anakimbilia NANI KAANZA KUONA JUA.

4. NYIMBO.

Hapa wakazuia kuimba jikoni, swaga walizoleta ni kwamba eti utaoa mzee, ina maana hawakuona sababu nyingine zaidi ya kuoa mzee?.... haikuwa kweli bana.

5. MRUKO.

Kwamba ukiwa umekaa mtu akakuruka basi unakuwa mfupi,. nyie..... hivi kuna uhusiano gani kati ya mruko na ufupi? tuwaombe kikao au tuwajaushie?

Zipo hadithi nyingi, ambazo zote haziwezi kuenea hapa tukisema tuzichambue, lakini hizo chache huenda zimekukumbusha jambo.

Sema mkubwa huwa hakosei, wao walitumia mbinu hizi kutufanya tuwe na subira, tuwe wachapa kazi, umakini katika mambo nk, lakini kikubwa kwa baadhi ya hadithi walitaka tufanye upembuzi wa mambo.

Na waliepuka mengi, mfano fikiria mzee anarudi nyumbani anaanza kukohoa nyumba ya tatu kabla ya kufika kwake, hapo home lazima mjiweke sawa kwa kila jambo mkijua mwenye mji anarejea, hata mafumanizi hayakuwepo kivile.

Sasa siku hizi jitu linakuja linanyata, ili mradi lipate sababu lianzishe ugomvi na ndio maana visukari ni vingi, visasi visasi lukuki na ngumi za kutosha tunazikana kwa mengi sana ambayo yanaepukika.

Wasalaam.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.