Skip to main content

KAHAMA WAZINDUA CHANJO YA POLIO, WATOTO 145,820 KUFIKIWA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

KAHAMA WAZINDUA CHANJO YA POLIO, WATOTO 145,820 KUFIKIWA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga inatarajia kuwafikia watoto 145,820 kwa ajili ya kuwapatia chanjo ya Polio, huku watoa huduma wakitarajiwa kuwafikia watoto hao sehemu tofauti ikiwa ni Pamoja na Nyumba kwa nyumba, Sokoni, Shuleni, Stendi za mabasi pamoja na vituo vya kulelea watoto.

Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa  Kahama, Dkt. Herry  Sylivester amesema  hayo kwenye uzinduzi wa utoaji wa chanjo huku akieleza watoto wanao takiwa kupata chanjo ni wale wenye umri chini ya miaka kumi.

“Manispaa ya Kahama tunatarajia kuwafikia watoto 145,820 wenye umri chini ya miaka kumi kupitia chanjo ya polio na tunataraji kupita nyumba kwa nyumba, stendi za mabasi,sokoni na kwenye vituo vya kulelea watoto yatima pamoja na kliniki,” amesema Dkt. Sylivester.

Dkt. Sylivester ameongezea kuwa uhamasishaji umefanyika kwa njia mbalimbali ili kuweza kuwafikia walengwa kupata chanjo ya polio, huku akisema mtoto asipopata chanjo hiyo na akipata ugonjwa wa polio unaweza kumsababishia ulemavu wa kudumu wakati mwingine kifo.

“Tumehamsisha sana wazazi kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo hii,Mtoto asipopata chanjo ya polia kuna uwezekao mkubwa wa kupata ugonjwa wa Polio ambao madhara yake unaweza kusababisha ulemavu wa kudumu na wakati mwingine kupelekea kifo kwa mtoto,” ameongeza Dkt. Sylivester.

Kwa upande wao, baadhi ya wazazi ambao watoto wao wamepatiwa chanjo hiyo akiwemo Rehema Mngaya na Christina Lucas wameishukuru serikali kwa kutoa chanjo hiyo ambayo itawasaidia watoto wao wasipate ugonjwa wa polio.

“Tunaishukuru sana Serikali kwa kutoa chanjo hii kwa watoto wetu, Chanjo hii itawasaidia watoto wetu wasipate ugonjwa wa polio,tuwaombe na wazazi wengine waachane na Imani potofu juu ya chanjo hii na badala yake wawalete watoto wao kupata chanjo,” wamesema Mngaya na mkazi wa manispaa ya Kahama.

Vimelea vya ugonjwa wa polio vimebainika mkoani Mwanza kwenye majitaka  hili iliyopelekea Serikali kuchukua jukumu la utoaji wa chanjo kwa  mikoa saba ya Kanda ya Ziwa, ikiwa hapa nchini Tanzania mgonjwa wa polio mara ya mwisho alibainika mwaka 1996.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.