Skip to main content

KAHAMA KWAWAKA MADEREVA NAO WAGOMA

Katika hali isiyo ya kawaida madereva wa mabasi ya masafa marefu yanayoanza safari zake Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga kwenda Mikoa ya jirani leo wamegoma kusafiri wakishinikiza Serikali kuwapunguzia vikwazo wanavyokutana navyo Barabarani ikiwemo kufungiwa leseni zao mara kwa mara.

KAHAMA KWAWAKA MADEREVA NAO WAGOMA
Studio Narration JAMBO FM

KAHAMA KWAWAKA MADEREVA NAO WAGOMA

0:00 --:--

Katika hali isiyo ya kawaida madereva wa mabasi ya masafa marefu yanayoanza safari zake Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga kwenda Mikoa ya jirani leo wamegoma kusafiri wakishinikiza Serikali kuwapunguzia vikwazo wanavyokutana navyo Barabarani ikiwemo kufungiwa leseni zao mara kwa mara.

Jambo Fm imefika katika kituo cha mabasi Kahama na kushuhudia umati wa abiria,madereva na wapiga debe wakiwa wamekaa wakisubiri hatma ya safari zao Kwenda Mikoani.

Kwa mujibu wa baadhi ya madereva wamesema kuwa wameamua kugoma baada ya kuona manyanyaso yamezidi barabarani yakiwemo kupigwa faini za mara kwa mara,Kufungiwa leseni zao na kutopata ushirikiano kutoka kwa vyombo vinavyosimamia usalama barabarani.“Ndugu mwandishi sisi madereva tunapitia changamoto nyingi sana barabarani kutwa nzima tunatozwa faini kila tunapopita,tumeomba muda mrefu kusikilzwa kero zetu lakini hadi sasa hakuna,leseni zetu zinafungiwa mara kwa mara na mbaya zaidi tunapoomba vikao na wahusika hatusikilizwi” Wamesema Madereva hao.

Wameiomba Serikali kurudisha mfumo wa kidhibiti mwendo (Speed Gavana)ambayo ilikuwa ni njia sahihi kwao na kuomba leseni zao zifungiwe na Mahakama na si Jeshi la Polisi kama ilivyo sasa .

“Ule utaratibu wa Speed Gavana tunaomba urudishwe ili dereva awe na kazi ya kulinda usalama barabarani na siyo kila muda aangalie mita ya speed,Pia na hawa askari wapunguze kamatakamata barabarani na kutufungia leseni” Wameongeza madereva hao.

Baadhi ya abiria waliokuwa katika kituo hicho kwa ajili ya safari wamesema kuwa wamepata shida kutokana na kila msafiri kuwa shida yake ikiwemo matibabu,misiba na hata biashara ila wamekwama kuendelea na safari huku wengine wakiwa hawana msaada wa chakula.

“Nilikuwa na safari saa kumi alfajiri ila hadi sasa niko hapa mi naelekea Dodoma nampeleka mama yangu anaumwa lakini hadi sasa sijui nifanye nini na hali ya mama ni mbaya,Kuna wengine wanaenda Kununua bidhaa za dukani na nilikuwa nisafiri usiku kesho jioni nirudi lakini sasa nimekwama hapa hatujui nini tufanye” Wamesema abiria hao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wasafirishaji Kahama Salumu Said amesema kwa sasa wanapokea abiria bila kuwakatia tiketi kwa sababu hawajui hatma ya mabasi hayo kama yatatoka au hayatatoka na kuongeza kuwa kwasasa wanaendelea kuwaelekeza abiria sehemu za huduma mbalimbali ikiwemo sehemu ya chakula na kuiomba Serikali kutoa suluhisho la mgomo huu haraka ili kuwanusuru abiria.

“Hali ni kama hii unavyoioana ndugu Mwandishi tupo hapa na abiria toka saa kumi usiku hakuna gari iliyotoka na magari yote yanayoingia yakifika hakuna kuendelea na safari,sisi kwa sasa tunachofanya tuna wapokea abiria japo hatuwakatii tiketi maana hatujui mgomo huu utaisha saa ngapi,kwasasa jitihada zetu ni kuzidi kuwaelekeza watu sehemu za huduma kama migahawa pamoja na sehemu za kujisaidia huku tukisubiri suluhisho la mgomo huu” Amesema Salum.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.