Skip to main content

KAGERA YAWEKA MIKAKATI KUKABILIANA NA UDUMAVU KWA WATOTO.

Mkoa wa Kagera umeweka mikakati sita kupitia Mkataba wa Lishe kwa lengo la kukabiliana na tatizo la utapiamlo na udumavu kwa watoto pamoja na jamii kwa ujumla.

KAGERA YAWEKA MIKAKATI KUKABILIANA NA UDUMAVU KWA WATOTO.
Studio Narration JAMBO FM

KAGERA YAWEKA MIKAKATI KUKABILIANA NA UDUMAVU KWA WATOTO.

0:00 --:--

Mkoa wa Kagera umeweka mikakati sita kupitia Mkataba wa Lishe kwa lengo la kukabiliana na tatizo la utapiamlo na udumavu kwa watoto pamoja na jamii kwa ujumla.

Afisa Lishe wa Mkoa wa Kagera, Joanitha Jovin, amesema hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe katika kikao cha lishe cha mkoa, akieleza kuwa mkoa umefanikiwa kutekeleza asilimia 89 ya afua za lishe katika kipindi cha Julai 2025 hadi Juni 2026.

Jovin amesema utekelezaji huo umeambatana na ongezeko la upatikanaji wa chakula shuleni kutoka asilimia 75 hadi asilimia 80, hali ambayo amesema inachangia kuboresha lishe na afya ya watoto wanaoendelea na masomo.

Amesema mafanikio hayo yamechangiwa pia na kuongezeka kwa ushiriki wa wadau mbalimbali katika utekelezaji wa afua za lishe, hatua inayolenga kuhakikisha jamii inapata elimu na huduma muhimu za lishe.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Ramadhani Kido, amezitaka halmashauri zote mkoani humo kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na udumavu.

Kido amesema udumavu unaweza kuathiri ukuaji na maendeleo ya watoto, hivyo kuna umuhimu wa kuweka mikakati ya kuhakikisha watoto wanapata lishe bora na huduma muhimu za afya.

Amesema takwimu za mkoa zinaonesha kuwa asilimia 34 ya watoto mkoani Kagera wanakabiliwa na udumavu, akisisitiza umuhimu wa kuimarisha upatikanaji wa lishe bora kwa watoto na jamii kwa ujumla.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.