Skip to main content

KAGERA YAONGOZA KWA MAUAJI NCHINI, POLISI WATAJA SABABU

Na Clavery Christian - Kagera.

KAGERA YAONGOZA KWA MAUAJI NCHINI, POLISI WATAJA SABABU

Na Clavery Christian - Kagera.

Jeshi la Polisi mkoani Kagera limesema mkoa huo unaongoza kwa matukio ya mauaji nchini, hali inayolifanya jeshi hilo kuongeza juhudi za kuyakabili na kuyapunguza kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, SACP Blasius Chatanda alisema matukio hayo yamekuwa yakichangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo migogoro ya kifamilia, wivu wa mapenzi pamoja na matumizi ya pombe kupita kiasi.

Amesema, Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu kuhakikisha linadhibiti hali hiyo kwa kushirikiana na wananchi, viongozi wa dini pamoja na serikali za mitaa ili kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yote ya mkoa huo.

Aidha, ametoa onyo kali kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia, hususan ubakaji, akibainisha kuwa sheria zimeanza kuchukua mkondo wake ambapo baadhi ya watuhumiwa wamehukumiwa adhabu kali ikiwemo kunyongwa hadi kufa, huku wengine wakipatiwa vifungo vya muda mrefu wa hadi miaka 30 jela.

“Hatutasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya kikatili. Sheria ipo wazi na tutahakikisha inasimamiwa kikamilifu ili kulinda usalama wa wananchi,” amesema Kamanda Chatanda.

Aidha, amewahimiza wananchi kutoa taarifa kwa wakati kuhusu viashiria vya uhalifu ili kusaidia juhudi za kudhibiti matukio hayo kabla hayajatokea.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.