Skip to main content

KADOGOSA AONGEZA TABASAMU KWA WANAFUNZI SEKONDARI YA IBULYU

Na Saada Almas, Bariadi - Simiyu.

KADOGOSA AONGEZA TABASAMU KWA WANAFUNZI SEKONDARI YA IBULYU

Na Saada Almas, Bariadi - Simiyu.

Mbunge wa Jimbo la Bariadi Vijijini, Masanja Kadogosa amekoleza vicheko kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Ibulyu kata ya Sakwe wilayani Bariadi mkoani Simiyu baada ya kuchangia viti 100, ili Wanafunzi hao waweze kuhudhuria vyema masomo yao kila siku bila kukwepa.

Awali wakazi wa kijiji cha Ibulyu wakiwemo wanafunzi waliosoma shuleni hapo miaka ya nyuma waliungana na diwani wa kata hiyo Charles Nduhi na kufanikiwa kujichangisha fedha zilizofanikisha kupata viti 100 na baada ya mwakilishi wa jimbo hilo kusikia juhudi hizo ameunga mkono kwa kuongeza viti 100 vinavyoweka idadi ya viti 200 kati ya uhaba wa viti 250 uliokuwepo.

Akikabidhi viti hivyo Katibu wa mbunge huyo Deogratius Matogo amesema kuwa faraja kubwa iliyopo kwa Kadogosa ni kuona shule zote zinapata mahitaji stahiki ya kumfanya mtoto apate elimu yake inavyostahili bila kuwa na vikwazo.

“sisi kama ofisi ya Mbunge tunafarijika kuona maendeleo katika sekta zote hasa elimu na kufika hapa ni kutimiza azma ya mbunge wenu ya kuhakikisha anaunga mkono juhudi za wananchi wapenda maendeleo pamoja na kuboresha mazingira ya wanafunzi kupata elimu,” amesema Matogo.

Ameongeza kuwa, ”tutaendelea kuwashika mkono kwa kila jambo ambalo litafika mezani kwetu kutoka kata hii na jimbo zima kwa ujumla lakini niwaombe wanafunzi viti hivi mvitumie na mvitunze kwani ninyi mnapopata elimu bora nyie wanapata ni wazazi wako na jamii nzima kwa hiyo mzithamini jitihada hizi.”

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Sakwe, Charlea Ndui Lyaganda amewataka wazazi kuendelea kujitoa kwa hali na mali kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za serikali za kimaendeleo huku wakiwa mabalozi wa kweli kwa wazazi wengine.

“Wazazi wenu wamenichagua niwe mwenyekiti wa maendeleo ya kata hii na mazingira ya wanafunzi ni moja ya maendeleo niwahakikishie ndani ya miaka mitano ambayo nitawatumikia nitahakikisha hakuna shule ambayo itakosa viti, wapo wazazi ambao wameuza hadi  mifugo kuchangia viti kuhakikisha mnasoma  vizuri,” amesema Ndui.

“bado tumebaki na uhaba wa meza 148 niwahakikishie kama umeweza kuchangisha viti utaendelea kuhangisha meza lengo ni kufua kabisa uhaba huu,shule hii imetoa wahasibu,imetoa walimu,imeoa wakandarasi tuake nini tena? lazima tuboreshe mazingira mazri ili tupate watumishi wazuri zaidi wa serikali yetu,” ameongeza Ndui.

Akitoa taarifa ya shule hiyo mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Ibulyu Mwl. Njile Madaha amesema kuwa viti hivyo viasaidia kupunguza utoro uliokuwepo kwa baadhi ya wanafunzi na kuwasihi wazazi kuendeleo kujitoa pale wanapo hiaika katika kuchangia shule hiyo ili waweze kumaliza uhaba wa meza 148 uliopo sasa.

Hata hivyo, Afisa Elimu Kata ya Sakwe Mniko Paul amesema katika shule sita za kata hiyo bado kumekuwa na upungufu wa madawati ,meza na viti hali inayopelekea kuwashirikisha wazazi kujitolea kuchangia, ili waoto wasome katika mazingira mazuri.

“Tuna shule tatu za Sekondari na 3 za msingi na bado uhaba upo japokuwa nipongeze mwamko wa wazazi pale tunapowagusia suala la kuchangia huwa wanatupokea kwa moyo na kujitoa kwa kila hali, hii inawajenga vyema hata wanafunzi badala ya kufikiria atakaa wapi akifika shuleni anakuwa anapeleka mawazo yake katika masomo tu,” amessma Mniko.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.