Skip to main content

JUNTA YAMNG’OA AFISA WAKE WA NGAZI YA JUU

Jopo la muungano wa Kijeshi (JUNTA) limemfuta Kazi Mshauri Mkuu wa wa Kijeshi wa muungano huo.

JUNTA YAMNG’OA AFISA WAKE WA NGAZI YA JUU
Studio Narration JAMBO FM

JUNTA YAMNG’OA AFISA WAKE WA NGAZI YA JUU

0:00 --:--

Jopo la muungano wa Kijeshi (JUNTA) limemfuta Kazi Mshauri Mkuu wa wa Kijeshi wa muungano huo.

Mkuu wa serikali ya muungano wa kijeshi Africa magharibi (JUNTA), ambae pia ni kiongozi wa kijeshi wa Guinea Bissau Jenerali Horta N'tam ametangaza rasmi kumfuta kazi afisa wake Mwandamizi wa Serikali ya kijeshi, aliyenasibishwa kuwa na ukaribu na Rais aliyeondolewa madarakani Umaro Sissoco Embaló.

Kwa mujinu wa N'tam uamuzi huo umechukuliwa ikiwa ni kile alichoeleza kama mwendelezo wa mabadiliko makubwa yanayofanywa katika idara za ulinzi na usalama tangu kuanguka kwa serikali ya Rais Umaro Sissoco Embaló.

Luteni Jenerali Fati, ambaye aliwahi kuhudumu kama Waziri wa Ulinzi pamoja na mshauri wa kijeshi wa Embaló, ameondolewa madarakani kutokana na kile kilichotajwa kama "athari ya mara moja" kulingana na amri ya uongozi wa muungano wa kijeshi (JUNTA).

Kwa mujibu wa duru kutoka ukanda wa Africa Magharibi hatua hii inajiri wakati kumeshuhudiwa mfululizo wa kufutwa kazi kwa maafisa waandamizi wa usalama wanaohusishwa moja kwa moja na rais huyo wa zamani, ambaye kwa sasa yupo uhamishoni nchini Morocco.

Hata hivyo Jopo hilo la muungano wa kijeshi (JUNTA) ililichukua madaraka mnamo Novemba 26, 2025 siku moja kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais na wabunge.

Kupinduliwa kwa Embaló na kusimamishwa kwa mchakato wa uchaguzi kulizua mashaka miongoni mwa wachunguzi wa kimataifa, baadhi yao wakihisi moja kwa moja kwamba Rais Embaló mwenyewe huenda aliratibu mapinduzi hayo ili kuzuia kushindwa katika uchaguzi aliokuwa akielekea kuukosa.

Kufuatia hayo hatua za hivi karibuni zilizochukuliwa na uongozi wa kijeshi zinaonyesha wazi kujitenga na kiongozi huyo wa zamani. Huku maafisa wengi wa walinzi wa Rais na makamanda waandamizi waliokuwa karibu naye wanaendelea kuondolewa kwenye nyazifa kubwa na zenye ushawishi.

Hadi sasa bado uongozi wa kijeshi ungali kutwaa madaraka ingawa jopo hilo la kijeshi liliahidi kuandaa uchaguzi wa urais na ubunge mnamo Desemba 6 ili kurudisha utawala wa kiraia, Mamlaka ya Uchaguzi ya Kitaifa wiki iliyopita ilitangaza kuwa "mazingira bado hayajaruhusu kufanyika kwa uchaguzi huo."

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.